Category Archives: Top Stories

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi 3 kama ifuatavyo;

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.

Dkt. Shein anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Barnabas A. Samatta ambaye anamaliza muda wake.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Dkt. Mwakyembe anachukua nafasi ya Bi. Mariam Joy Mwaffisi ambaye amemaliza muda wake.

Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Gaudentia Mugosi Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Bi. Gaudensia Mugosi Kabaka anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 24 Novemba, 2020.

 

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB) KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Palamagamba Kabudi (Mb) kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kuwa Waziri wa Fedha na Mipango katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020