Daily Archives: July 13, 2014

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE MGENI RASMI KWENYE KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 75 YA TANZANIA ASSEMBLIESE OF GOD (TAG) MBEYA

S

 

 

SONY DSC

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili uwanja wa ndege Songwe Mbeya kwa ajili ya kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya miaka 75 ya kanisa la  Tanzania Assembliese of God (TAG) Mbeya  Julai 13,2014

SONY DSC

 

Vijana wa halaiki wanogesha maadhimisho ya miaka 75 ya Tanzania assembliese of god katika uwanja wa Sokoine  Mkoani Mbeya julai  13,2014

SONY DSC

maadhimisho ya miaka 75 ya Tanzania Assembliese of God  yalifunguliwa kwa wimbo wa taifa ulioongozwa na kikosi cha bendi cha jeshi la Magereza katika uwanja wa Sokoine  Mkoani Mbeya julai  13,2014

zaxsc

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye  kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa la Tanzania Assemblies of God  katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014

xxclnci

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha  Tanzania Assemblies of God (TAG) akiwa na  Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya  Julai 13, 2014

1

 

tuzo

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa tuzo na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya  Julai 13, 2014

ZIARA YA RAIS KIKWETE WILAYA YA PANGANI – TANGA

fukwwe

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia fukwe za mji wa Pangani wakati akivuka kwenda kata ya Bweni kwa kutumia kivuko kipya M.V.Pangani Julai 11,2014 .Mji wa Pangani uko katika hatari ya kumezwa na bahari kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji kulikosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

MAJIII

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua bomba la maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Bweni wilayani Pangani mkoa wa Tanga Julai 11,2014

MBUNG

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mbunge wa Pangani Mhe.Saleh Pamba wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Kipumbwi huko Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Julai 11,2014

hdkdj

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakinunua samaki katika kibanda huko Bweni Wilaya ya Pangani Julai 11,2014 wakati Rais alipokwenda kuzindua mradi wa maji na kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa maabara shule ya sekondari Kipumbwi.

unnamed

 

mmmm

Muuza samaki akifunga samaki aliyenunuliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete  katika kibanda huko Bweni Wilaya ya Pangani Julai 11,2014 wakati Rais alipokwenda kuzindua mradi wa maji na kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa maabara shule ya sekondari Kipumbwi. BONYEZA HAPA KUPATA VIDEO  http://youtu.be/GzqCY1CtZYA

1

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakiangalia mandhari ya mji wa Pangani wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo.Sehemu kubwa ya mji huo imo katika hatari ya kumezwa na bahari kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali imeahidi kujenga ukuta pembezoni mwa mto Pangani ili kuzuia athari za kimazingira kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji.

2

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipitia moja ya hotuba zake akiwa ndani ya kivuko kipya cha MV Pangani II wakati akivuka mto Pangani kutoka Tarafa ya Bweni kuelekea Pangani mjini wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Pangani. Rais Kikwete ambaye alikuwa mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya wiki moja alihitimisha ziara hiyo jana ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa serikali itajenga kivuko kingine kwenye mto huo chenye uwezo mkubwa zaidi ili kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii wilayani humo.

3

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya majumuisho wakati akihitisha ziara yake ya kikazi ya wiki moja mkoani Tanga ambapo alizindua na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameziagiza Halmashauri zote nchini kutenga  ardhi kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ajili ya kujenga nyumba za bei nafuu kote Nchini.

Rais Kikwete ametoa maagizo hayo leo mjini Tanga wakati akifanya majumuisho ya ziara yake katika Mkoa wa Tanga.
Rais amesema nyumba za bei nafuu zikijengwa  zitatoa nafuu na kuondoa tatizo la makazi kwa  wafanyakazi na wananchi wenye nia ya kumiliki nyumba na pia itapendezesha Halmashauri hizo.

Katika ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga ambayo imefanyika kwa awamu mbili, Rais ametembelea Wilaya zote za Handeni, Kilindi, Lushoto, Korogwe, Mkinga,  Muheza, Pangani na Tanga.

Rais pia amewataka viongozi kote nchini kusimamia na kuhakikisha kuwa tatizo la watoto kutomaliza shule linasimamiwa na kushughulikiwa ipasavyo kwa sababu huo ndiyo msingi wa maendeleo katika Taifa letu.

“Viongozi lazima kusimamia suala la elimu kwani hapo ndipo tunapowekeza kwa ajili ya hatma ya vizazi vyote” amesema na kuongeza kuwa wasiokuwepo shule watafutwe na wazazi waulizwe walipo watoto hao walioacha shule.

Rais amezitaka Halmashauri zote zikae na kujadili hali ya mahudhurio ya watoto shuleni na kutoa taarifa Serikali Kuu mapema.

Akiwa Mkoani Tanga, Rais amesema Serikali itaendelea kutekeleza ahadi zake na kusimamia zilizoanza ili zikamilike kwa wakati. Kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu, Rais Kikwete amesema hatma yake iko katika matokeo ya maamuzi ya Bunge la Katiba na pia kutegemea aina gani ya serikali itakayopendekezwa, ambapo kama Bunge la Katiba litaamua kuwa na Serikali mbili, uchaguzi unaweza kusogezwa mbele kidogo kwa ajili ya matayarisho na kisha kufanyika, ila kama itaamuliwa kuwa na Serikali tatu, uchaguzi huo utategemea Katiba ya Tanganyika ambayo itabidi  iandikwe kwanza.