Daily Archives: July 17, 2014

ZIARA YA RAIS JAKAYA KIKWETE MKOA WA RUVUMA WILAYA YA SONGEA MJINI

efkekk

Rais Jakaya Kikwete akipokelewa na mkuu na Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ,kwa ajili ya kuanza ziara ya kukagua shughuli za Maendeleo Mkoani humo Julai 17,2014

ANGALIA VIDEO JINSI RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ALIVYOWASILI SONGEA MJINI KWA ZIARA YA SIKU SABA MKOA WA RUVUMA NA KUKAGUA HIFADHI YA CHAKULA NA KUFUNGUA GHALA LA KUHIFADHI CHAKULA NA KISHA KUFUNGUA NYUMBA ZILIZOJENGWA KWA GHARAMA NAFUU ZA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)

g5t5y5y

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ghala la Mahindi mjini Songea leo wakati wa mwanzo wa ziara yake ya kikazi Mkoani Ruvuma ambapo alizindua rasmi ghala hilo.Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa wakala wa hifadhi ya taifa ya Chakula Bwana Charles Walwa.Rais Kikwete amewasii Mkoani Ruvuma  julai 17,2014

2

 

3

 

1

 

6

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ghala la Mahindi mjini Songea wakati wa mwanzo wa ziara yake ya kikazi Mkoani Ruvuma ambapo alizindua rasmi ghala hilo Julai 17,2014

sccdcc

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la msingi wakati wa ufunguzi wa nyumba  zilizojengwa kwa gharama nafuu na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)  Mkuzo wilayani Songea mjini Mkoani Ruvuma Julai 17,2014 .Kushoto ni  kaimu Mkurugenzi wa NHC Bwana David Misonge Shambwe na wwapili kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na makazi Prof.Anna Tibaijuka.

scsccdc

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi nyumba zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC  Mkuzo, wilayani Songea mjini mkoani Ruvuma Julai 17,2014. Kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof.Anna Tibaijuka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Bwana David Misonge Shambwe, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said Mwambungu

D92A2347

Aina ya  nyumba zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC  Mkuzo, wilayani Songea mjini mkoani Ruvuma 

D92A2262

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akabidhi mashine za kufyatulia matofari kwa vijana wajasiliamali wawilaya ya  songea mjini mashine zilizotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)  Julai 17,2014 

3

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na kaimu Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Bibi Mary Mosha wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa ufunguzi wa jengo la ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma  Julai 17,2014

2

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Ruvuma  mjini Songea Julai 17,2014

pccb jengo

  Jengo la ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Ruvuma  mjini Songea iliyofunguliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Julai 17,2014

D92A2565

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa ufunguzi  rasmi wa ofisi za taasisi ya kuzuia rushwa TAKUKURU mkoa mjini Songea Julai17,2014.Kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Mary Mosha.

kaimu pccb

kaimu Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Bibi Mary Mosha  akisoma taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa jengo la ofisi ya TAKUKURU lililofunguliwa na Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete Julai 17,2014

 

 

 

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGEA NA WASANII NYOTA WA FILAMU NA MUZIKI KUTOKA MAREKANI

 

 

7

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka  Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni na  Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto)  na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.


5

 

2

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa muziki na filamu kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni   Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.

3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia simu yake ya mkononi kuwaonesha vivutio vya kitalii wasanii nyota wa muziki na filamu wa Kimarekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni   Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu Julai 14, 2014 amekutana na kundi la wasanii kutoka Marekani lililowasili nchini usiku wa Alhamisi, Julai 10, 2014, kwa ajili ya kuendesha mafunzo kwa wasanii wa Tanzania kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mjini Dar es Salaam.

Wasanii hao ni pamoja na  Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group.

Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.

Kiasi cha wasanii 250 walishiriki semina hiyo inayoitwa Mafunzo ya Uendelezaji Usanii. Hiyo ilikuwa ni kutimiza ahadi aliyotoa Rais Kikwete kwa wasanii wa Tanzania kuwa atachangia kuinua kiwango cha ujuzi na weledi wao kwa kuwaandalia mafunzo yatayoendeshwa na magwiji wa sanaa kutoka Marekani sasa imetimia.

Akizindua Kampeni ya Uzalendo kwa Vijana inayoendeshwa na Muungano wa Wasanii Tanzania kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwezi uliopita, Juni 14, 2014, Rais Kikwete aliahidi kuchangia kuinua kiwango cha usanii na weledi wa wasanii wa Tanzania kwa kusaidia kuandaa mafunzo yatakayoendeshwa na wasanii maarufu kutoka Marekani.

Mbali na kuendesha shughuli za mafunzo ya wasanii ambazo wamekuwa wakizifanya kwa makundi madogo madogo tokea walipowasili nchini, pia wanamuziki hao wa Marekani na kundi la wapiga picha watatembelea sehemu mbali mbali  nchini, hasa kwenye vivutio vya watalii, ambako watapiga picha na kuandaa vipindi vya kuitangaza Tanzania katika vyombo vya habari vya Marekani.