Daily Archives: July 17, 2014

RAIS KIKWETE AKABIDHI BENDERA TIMU YA TAIFA YA RIADHA ITAYOSHIRIKI MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA HUKO GLASGOW, SCOTLAND

1

 

2

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.

3

 

4

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.

5

Wakimsikiliza kwa makini Rais Kikwete ni wachezajina viongozi wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.

6

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi ya kukabidhi bendera iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM

wdefef

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM jijini Dar es salaam Julai 16,2014

unnamed

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue leo tarehe 16 Julai, 2014 amekutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. Thomas cha Minnesota, Marekani wanaotembelea Tanzania kujifunza uzoefu wa Tanzania katika masuala ya kiuongozi na anuwai ya tamaduni. Wanafunzi hao ambao kwa idadi yao ni wanafunzi 14 wanaochukua Shahada za Uzamivu na Uzamivu katika masuala ya Uongozi wa Kimataifa pamoja na Wakufunzi wao wawili, Dkt. Jean Pierre Bongila na Dkt. Artika Tyner.

 Mkutano huu ni mwendelezo wa mkutano kama huu ambao Katibu Mkuu Kiongozi aliufanya mwaka jana na kundi jingine la wanafunzi kutoka Chuo hicho ambapo aliwapa uzoefu wa uongozi na anuwai ya tamaduni katika Tanzania, Afrika na katika medani za kimataifa.

             Kwa kutambua umuhimu wa nasaha walizozipata wanafunzi wa mwaka jana, Chuo hicho kiliomba na kukubaliwa fursa nyingine ya kuonana na Katibu Mkuu Kiongozi. Ziara ya wanafunzi hao ilianzia Arusha tangu tarehe 12 Julai, 2014 na itamalizika tarehe 17 Julai, 2014

           Pamoja na kupata fursa ya kuonana na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Arusha, wanafunzi hao walipata pia muda wa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Arusha na baadaye Zanzibar. Na matarajio ni kuwa wanafunzi hao watakuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania sehemu mbalimbali za dunia watakakokwenda kufanya kazi.

             Kwa ujumla, wanafunzi wamepata fursa nzuri ya kuuliza maswali yaliyogusa maeneo yote yanayohusu uongozi, siasa, uchumi, elimu, afya na utamaduni ambayo yalipata ufafanuzi wa kutosha kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.