Daily Archives: July 22, 2014

ZIARA YA RAIS JAKAYA KIKWETE MKOANI RUVUMA WILAYA YA TUNDURU

ANGALIA VIDEO JINSI RAIS KIKWETE ALIVYOFUNGUA NYUMBA ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA KIJIJI CHA MATEMANGA WILAYA YA TUNDURU

utepe 1

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua mradi wa nyumba za watumishi wa afya zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation katika hafla iiyofanyika katika kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma Julai 22,2014 Jumla ya nyumba 480 zinajengwa katika halmashauri 48 nchini na miongoni mwa nyumba hizo 40 zipo katika mkoa wa Ruvuma.Taasisi ya Benjamin Mkapa iliingia mkataba na Wizara ya Afya kutekeleza mradi wa miaka mitano(2011-2016) wa uimarishaji wa mifumo ya Huduma za afya chini ya ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na ukimwi,kifua kikuu na Malaria(Global Fund).Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin W.Mkapa Dkt.Ellen Senkoro, Mbunge wa Jimbo la Tunduru Mhandisi Ramo Makani, Meneja wa Portfolio, Mfuko wa Dunia wa Kupambana na ukimwi,kifua kikuu na Malaria Bi. Tatajana Peterson, Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof.Anna Tibaijuka, Naibu Waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri, Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Kebwe Stephen  Kebwe, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Saidi Mwambungu

r

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin w.Mkapa Dkt  Ellen Mkondya Senkoro(kushoto) akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete michoro na ramani za nyumba za watumishi wa afya zilizojengwa na taasisi hiyo wkati hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo uliofanyika katika kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru Julai 22,2014 Watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na wane kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka.

haadara

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa kijiji cha Matemanga wakati wa hafla ya uzinduzi nyumba 480 za watumishi wa umma zilizojengwa na Taaasisi ya Benjamin W.Mkapa kwa ushirikiano na Wizara ya Afya Julai 22,2014

D92A9730

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mbunge wa Tunduru mhandisi Ramo Makani, Balozi mdogo wa Japan Kazuyoshi Matsunaga na mwakilishi Mkazi wa Benki ya maendeleo ya Afrika(ADB) Bibi Tonia Kandiero wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua ujenzi Barabara ya kilometa 195.7 ya Matemanga Tunduru-Mangaka uliofanyika Tunduru mjini.Barabara hiyo imejengwa na serikali ya Tanzania kupitia wakala wa Barabara TANROADS ikisaidiwa na Benki ya mendeleo ya Afrika ADB na shirika la maendeleo la Japan JICA.Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika mjini Tunduru julai 22,2014D92A9760

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Matemanga-Tunduru hadi Mangaka yenye urefu wa kilometa 195.7 wakati wa hafla iliyofanyika mjini Tunduru Julai 22,2014 Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mbunge wa Tunduru Mhandisi Ramo Makani, Balozi mdogo wa Japan Kazuyoshi Matsunaga, Mwakilishi Mkazi wa ADB Bi.Tonia Kandiero na waairi wa Ujenzi John Pombe Magufuli. Barabara hiyoimejengwa na serikali ya Tanzania kupitia wakala wa Barabara TANROADS ikisaidiwa na Benki ya mendeleo ya Afrika ADB na shirika la maendeleo la Japan JICA.

D92A0142 - Copy

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua maji katika kisima kuashiria kuzindua rasmi mradi wa Maji katika kata ya Nalasi wilayani Tunduru Julai 23,2014 Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande Bakari Nalicho,Wapili kulia anayepiga makofi ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu na kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

D92A0174

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata ya Nalasi Rehema Kassim Yakubu wakati alipokwenda kuzindua mradi wa maji katika kata hiyo iliyopo katika wilaya Tunduru Julai 23,2014 ANGALIA VIDEO YA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI NALASI na Shamrashamra za maelfu ya wakazi wa Tarafa ya NALASI liliko jimbo la TUNDURU Kusini walipompokea Rais JAKAYA KIKWETE ambaye safari yake hapa ilikua ni kufungua mradi wa Maji aliowaahidi mwaka 2010 katika Kampeni za UchaguzI Mradi huu umetekelezwa kwa zaidi ya shilingi milioni 400 na utavinufaisha vijiji vitatu vya NALASI BONYEZA HAPA 

D92A1165

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza balozi mdogo wa Japan Kazuyoshi Matsunaga Julai 23,2014 muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Tunduru-Mangaka  Matemanga mradi unaojengwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la kimataifa la maendeleo JICA.Kushoto ni mbunge wa Nanyumbu Dunstan Mkapa, wapili kushoto ni Waziri wa ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kulia ni Wairi wa Ardhi nyumba na mendeleo ya  makazi Profesa Anna Tibaijuka

D92A9704

wananchi wa Mangaka Wilaya ya Nanyumbu wakishuhudia uzindua wa ujenzi wa Barabara ya Tunduru-Mangaka  Matemanga mradi unaojengwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la kimataifa la maendeleo JICA Wakati Rais Kikwete alipokwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo Julai,23,2014