Daily Archives: August 4, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA WANAWAKE WATANZANIA WAJASIRIAMALI WAISHIO WASHINGTON

1Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa Ndugu Juster Mutakyawa mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani iliyoko Washington tarehe 3.8.2014.2Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Watanzania wanaoishi Washington kiitwacho TANO Ladies Ndugu Asha Hariz wakati alipotembelea ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani tarehe 3.8.2014.3 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kipeperushi kutoka kwa Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya  Help for Underserved Communities  (HUC) ya nchini Marekani Ndugu Zawadi Sakapalla baada ya kupata taarifa ya huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo. Kampuni hiyo husaidia familia maskini kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa kuwachimbia visima pamoja na kutoa vifaa vya elimu kwa wanafunzi.4Baada ya kutembelea maonesho ya wanawake wajasiriamali Mama Salma Kikwete akifuatana na Afisa Tawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka kwenda kuweka saini kwenye kitabu cha wageni.5Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha wageni. Aliyesimama kushoto ni Bibi Lily Munanka, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.6Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitambulishwa kwa wana kikundi wa TANO Ladies. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti Asha Hariz, akifuatiwa na Asha Nyang’anyi, Isca Kauga, Juster Mutakyawa na Tumaini Kaisi aliyeshika kipaza sauti.7Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kikundi cha TANO Ladies cha nchini Marekani. Anayekabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya wanakikundi wenzake  Ndugu Juster  Mutakyawa.8 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani kwenye ukumbi wa ofisi ya ubalozi wetu mjini Washington tarehe 3.8.2014.

9Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani kwenye ukumbi wa ofisi ya ubalozi wetu mjini Washington tarehe 3.8.2014.

10

 

11

Baadhi ya wanawake wajasiriamali na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.