Daily Archives: September 2, 2014

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA AMANI NA USALAMA WA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA JIJNI NAIROBI SEPTEMBA 02,2014

2

 

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiteta jambo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi katika mkutano wa  Baraza la Amani na Usalama la nchi za umoja wa Afrika (AU) kwenye mkutano wa kuzungumzia masuala ya tishio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla septemba 02,2014

3

Nyimbo za AU na Kenya zikipigwa kabla ya  mkutano wa kuzungumzia masuala ya tishio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla  katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi September 2,2014k

 Katibu wa Rais Prosper Mbena  na Barozi wa Tanzania Nchini Kenya Batrida Buriani wakiingia kwenye mkutano wa kuzungumzia masuala ya tishio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla  katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi September 2,2014

 

 

RAIS KIKWETE AUNGANA NA WENZAKE MKUTANO WA UGAIDI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Septemba 2, 2014, ameungana na viongozi wengine wa Afrika na wajumbe kutoka nchi mbali mbali duniani kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) kujadili hatari na athari za ugaidi katika Bara la Afrika na namna ya kukabiliana nao. Katika Mkutano huo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta – Kenyatta International Convention Centre (KICC) mjini Nairobi, Kenya umefanyika chini ya uenyekiti wa Mwenyekiri wa sasa wa Baraza hilo, Mheshimiwa Idrisa Deby, Rais wa Chad. Nchi zote 15 wanachama wa Baraza hilo zimewakilishwa katika Mkutano huo wa siku moja na miongoni mwa Marais ambao walihudhuria mbali na Rais Kikwete na Rais Deby ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Mheshimiwa Goodluck Jonathan, Rais wa Nigeria, Rais wa Somalia, na mwenyeji wa Mkutano huo, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya. Rais Kikwete ambaye aliwasili mjini Nairobi usiku wa jana, Jumatatu, Septemba Mosi, 2014, baada ya kukatisha kwa muda ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Dodoma, alitarajiwa kuhutubia Mkutano huo baadaye jioni ya leo. Kikao cha ufunguzi cha mapema asubuhi, wajumbe walisikia hotuba kutoka kwa viongozi wanne wakianza na Rais Deby ambaye alitoa hotuba ya ufunguzi akifuatiwa na Rais Jonathan ambaye alizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Mheshimiwa Mohamed Abdulaziz, Rais wa Mauritania ambaye hakuweza kuhudhuria Mkutano huo.  Rais Jonathan ambaye nchi yake imeathirika mno kutokana na ugaidi wa Kikundi cha Boko Haram amesema kuwa ugaidi unashamiri katika Afrika kwa sababu ya kuongezwa nguvu na uhalifu mwingine wa kimataifa kama vile biashara ya dawa za kulevya, ujangili, biashara ya binadamu, biashara ya fedha haramu.  Amesema kuwa dunia na Afrika inahitaji mbinu nyingine za kukabiliana na ugaidi kwa sababu ya uhalifu huo kusaidiwa na uhalifu wa aina nyingine na ambazo unavuka mipaka ya nchi mbali  kwa urahisi zaidi. Naye Rais Kenyatta ambaye pia nchi yake imeathiriwa mno na ugaidi wa Kikundi cha El Shaabab, amesema kuwa Bara zima la Afrika linakabiliwa na ugaidi zikiwa nchi za eneo la Sahel za Chad, Mali na Libya, eneo la Afrika Mashariki ambalo linasumbuliwa na ugaidi wa El Shaabab na eneo la nchi za Nigeria na Cameroun, ambazo zinasumbuliwa na Boko Haram na eneo la Afrika ya Kati ambazo zinasumbuliwa na ugaidi wa Lord’s Army. Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika, Balozi Erasto Mwencha amesema kuwa uteuzi wa Jiji la Nairobi kuandaa Mkutano huo ni mwafaka kabisa kutokana na madhara ambayo Jiji hilo na nchi ya Kenya kwa jumla imekuwa inapitia kwa sababu ya mashambulizi ya ugaidi.

“Kwa pamoja tumekuja hapa kuelezea mshikamano wetu na ukaribu wetu kwa Kenya, wananchi wake na Serikali yake kutokana na mashambulzi ambayo yamekuwa yanaikumba nchi hii,” amesema Balozi Mwencha.

Mkutano huo pia umesikiliza Ripoti ya Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika  kuhusu aina, athari, hatari ya ugaidi na namna nchi hizo zinaweza, kwa pamoja, kukabiliana na kushinda balaa hilo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu,

DAR ES SALAAM. 

2 Septemba, 2014

 

 

 

 

 

 

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA NYUMBA ZA ZA MAKAZI ZA MEDELI DODOMA MJINI SEPTEMBA 01,2014

agdghfj

Rais Jakaya Kikwete akifungua Nyumba za  makazi za Medeli Dodoma Mjini Septemba 01,2014 zilizojengwa na shirika la nyumba la Taifa NHCBBBBBB

Rais Jakaya Kikwete akikagua Nyumba za  makazi za Medeli Dodoma Mjini Septemba 01,2014 zilizojengwa na shirika la nyumba la Taifa NHCP1030271

 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa  NHC  baada ya kufungua nyumba zilizojengwa na Shirika hilo Dodoma

RAIS KIKWETE ATEMBELEA WILAYA YA CHAMWINO KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA DODOMA AUGOSTI 30,2014

1

 Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde “Kibajaji”

2

 Rais Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani humo6

 Ujumbe toka kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Msanga5

 Ujumbe toka kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Msanga7

 

8

 Rais Kiwkete akiwapongeza wacheza ngoma wa Shule ya Msingi ya Msanga11

 Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe Fatma S. Ally akitoa taarifa ya Wilaya12  Watendaji wa Wilaya ya Chamwino wakiwa katika kikao na Rais Kikwete 13

 Rais Kikwete akitoa ushauri na maagizo kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali14

 Watendaji wa Wilaya wakisikiliza kwa makini15

 Mwalimu Silvanus Hosea wa shule ya Bwigiri ambaye ni mwalimu mwenye ulemavu wa macho akitoa maoni yake16

 Mwakilishi wa shirika la kimataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) akifafanua juu ya mradi wa chakula kwa wanafunzi mashuleni17

 Rais Kikwete akitoa ushauri wa njia bora za kuendeleza mradi wa chakula kwa wanafunzi mashuleni18  Vijana waliomaliza elimu ya juu na kuamua kujishuhghulisha na mradi wa kilimo wilayani Chamwino wakitambulishwa. Rais Kikwete ameahidi kuwapatia trekta ili kuongeza tija19

 Mmoja wa wataalamu wa miradi akitambulishwa 20

 Rais Kikwete akisalimiana na Mwalimu Silvanus Hosea wa shule ya Bwigiri21

 Rais Kikwete akisalimiana na wahandisi wa mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya Wilaya ya Chamwino22

 Sehemu ya mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashuari ya wilaya ya Chwamwino23

 Kikundi cha utamaduni cha kinamama kikitumbuiza katika sherehe za uwekaji wa jiwwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino24

 Wananchi wakifurahia katika sherehe za uwekaji wa jiwwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino25

 Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe Fatma S. Ally akimkaribisha Rais Kikwete na ujumbe wake26

 Katibu tawala wa Wilaya ya Chamwino akitoa muhtasari wa mradi wa ujenzi wa jengo la halmashauri ya wilaya hiyo27

 Mbunge wa jimbo la Chamwino Mh. Chibulunje akizungumza katika sherehe hizo ambapo alitangaza nia ya kutogombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao mwakani28

 Rais Kikwete akimpongeza Mbunge wa Chamwino Mhe Chibuluje kwa kutangaza hadharani nia yake ya kutogombea tena nafasi hiyo 29

 Rais Kikwete akizungumza na wananchi30  Rais Kikwete na Mbunge wa jimbo la Chamwino Mhe Chibuluje wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino31

 Vifijo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino32

 Rais Kikwete akipata maelezo ya  mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino33

jiwe la msingi la mradi34

 Rais Kikwete akilakiwa na walimu wa Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela alipowasili ili kuzindua  maabara ya masomo ya sayansi35

 Rais Kikwete akikaribishwa kwa ngoma  Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela alipowasili ili kuzindua  maabara ya masomo ya sayansi36

 Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde Kibajaji akiongea machache wakati wa sherehe za uzinduzi wa maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela 37

 Rais Kikwete akizungumza na wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela38

 Rais Kikwete akizindua maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela40

 Rais Kikwete akikata utepe kuzindua maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela41

 Rais Kikwete akiangala wanafunzi wakiwa mafunzoni baada ya kuzindua  maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela42

 Rais Kikwete akiangala wanafunzi wakiwa mafunzoni baada ya kuzindua  maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela43

 Wanafunzi wakiwa mafunzoni baada ya Rais Kikwete  kuzindua  maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela44

 Rais Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na walimu  baada ya kuzindua  maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela45

 Rais Kikwete akiwasili katika Shule ya Sekondari ya Mvumi Mission46

 Rais Kikwete akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mvumi Mission47

 Rais Kikwete akiwapa somo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mvumi Mission48

 Rais Kikwete katika picha na walimu na viongozi wa wanafunzi  Shule ya Sekondari ya Mvumi Mission49

 Rais Kikwete akiongea na wananchi baada ya kuwasili mvumi kuzindua mradi wa maji50

 Rais Kikwete akiongea na Mbunge wa Mtera Mhe Livingtsone Lusinde51

  Rais Kikwete  na Mbunge wa Mtera Mhe Livingtsone Lusinde wakizindua mradi wa maji wa Mvumi52

 Rais Kikwete akimtwisha ndoo mmoja wa wakinama baada ya kuzindua mradi wa maji wa Mvumi53

 Rais akilakiwa na umati wa watu alipowasili uwanja wa Mvumi kwa mkutano wa hadhara54

 Rais Kikwete akipokea zawadi ya mkuki na fimbo 56

 Rais Kikwete akimshukuru Mzee Manyweke kwa zawadi58

 Zawadi zaidi toka kwa wazee mashuhuri wa Mvumi59

 Rais kikwete akipata picha ya pamoja na wazee mashuhuri wa Mvumi 60

 Rais Kikwete akipewa zawadi ya mbuzi kutoka kwa vijana wa stendi ya basi ya Mvumi61

 Ngoma ya utamaduni62

 Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde akiongea na wananchi63

 Rais Kikwete akimpongeza Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde 64

 Rais Kikwete akihutubia wananchi65

 Umati wa wananchi wakimsikiliza Rais Kikwete67

 Rais Kikwete akipongezwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino66

 Rais Kikwete akipeana mikono na Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde

68

 Rais Kikwete akipeana mikono na Mhe Chibuluje69

Rais Kikwete akiagana na wananchi wa Mvumi.