Daily Archives: October 15, 2014

RAIS KIKWETE ATOA HATI YA URAIA KWA WALIOKUWA WAKIMBIZI WA BURUNDI OKTOBA 14, 2014

1nlnkk Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya jana,  Oktoba 14, 2014, alitoa Hati za Uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 162,000 ambao walikuwa wakimbizi kutoka Burundi na ambao wameishi nchini kwa miaka 42, tokea Mwaka 1972. Rais Kikwete ametoa Hati hizo katika shughuli fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ikiwa sehemu ya shughuli za Rais Kikwete katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo. Kwa niaba ya wenzao, Rais Kikwete ametoa Hati hizo kwa wakimbizi hao 19 wa zamani kwa niaba ya wenzao. Hapa ni Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa hati ya Uraia wa Tanzania Bi.Bizimana Nyakiki Naluka mmoja wa kati ya wakimbizi 162,000 kutoka Burundi waliopatiwa uraia wa Tanzania

3nbjj

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wakimbizi kutoka Burundi waliopatiwa hati za uraia wa Tanzania katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Tabora Oktoba 14 ,2014

2

wakimbizi hao wakiimba wimbo maalum kuonyesha furaha kwa kukubaliwa kupata Hati ya uraia wa Tanzania