Daily Archives: October 22, 2014

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA MABALOZI WA AFRIKA NCHINI CHINA OKTOBA 22, 2014

zxzxzx

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilkisha nchi zao nchini China wakati alipokutana nao jijini Beijing China Oktoba 22, 2014.Rais Kikwete yupo nchini China kwa ziara ya kiserikali2

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilkisha nchi zao nchini China wakati alipokutana nao jijini Beijing China Oktoba 22, 2014.Rais Kikwete yupo nchini China kwa ziara ya kiserikali

unnamed (16)

 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai ya mjini Beijing mara baada ya kuwasili nchini China kwa ziara ya kikazi tarehe 21.10.2014.
unnamed (18)

 Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa China National Offshore Oil Corporation Bwana Wang Yilin wakizindua rasmi mtambo mpya wa utafutaji wa mafuta na gesi baharini, Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014.
unnamed (19)
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania unaozuru nchini China wakiangalia vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na Shirika la  CNOOC la China katika kazi ya utafutaji wa mafuta na gesi baharini wakati walipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014.

unnamed (20)

 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akishirikiana na Mkewe Mama Salma Kikwete na Professa Li Songshan (kushoto kwa Rais Kikwete), Mwanzilishi wa Kijiji cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe 22.10.2014.

 

unnamed (21)

 Vifijo baada ya ufunguzi wa Kijiji cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe 22.10.2014.unnamed (22)
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya ngoma za asili ya Afrika zilizokuwa zikipingwa na vijana wa kichina mara baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha sanaa za Afrika huko Songzhuang tarehe 22.10.2014.
unnamed (23)
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama.
unnamed (26)
Waanzilishi wa Kijiji cha Sanaa za Afrika Professa Li Songshan na Mke wake Dkt. Han Rong wakimkabidhi zawadi ya mchoro wa  Tingatinga Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mke wake mara baada ya ufunguzi rasmi wa kijiji hicho tarehe 22.10.2014.