Monthly Archives: November 2014

RAIS KIKWETE ATOLEWA NYUZI KATIKA MSHONO-AFYA YAKE YAZIDI KUIMARIKA NOV.22, 2014

2

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri .Kulia kwake ni Daktari wa Rais
Profesa .Mohamed Janabi

 

 

JAJI MKUU AMJULIA HALI RAIS KIKWETE MAREKANI

unnamed-1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama  

unnamed-2

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland.  Jaji Mkuu yuko  Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. unnamed-4

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani  Dkt. Sweetbert Mkama ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman kwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014 unnamed-5

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Meja Jenerali Adolph Mutta ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman kwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014     unnamed-6

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein Katanga. ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014     unnamed-7

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe Ignass Kitusi  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014     unnamed-8

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyesindikiza   msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014   unnamed-9

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji wa Mahakama Ya Rufani Tanzania Mhe Ibrahim Juma  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014   unnamed-10

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  Jaji Mkuu na ujumbe wake wako  Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama.