Daily Archives: December 23, 2014

KATIBU MKUU KIONGOZI AMSIMAMISHA KAZI KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHARTI NA MADINI

Maonyesho ya Kilimo Nane Nane Kanda ya kati katika Viwanja vya NZUGUNI DODOMA-2014 (5)

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda Ndugu Eliakim Maswi,  Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.”

Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi utakapokamilika.

Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia imekariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana, Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:

“Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”

Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.

Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme (TANESCO) waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha tozo la uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzo la awali lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa (ICSID).

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

23 Desemba,2014

 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MSANII NASEEB ABDUL ‘DIAMOND’ IKULU, AWAPONGEZA YEYE NA IDRIS SULTAN KWA KUILETEA SIFA TANZANIA DESEMBA 23, 2014

unnamed-1 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha msanii Naseeb Abdul “Diamond”  na  kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014 

unnamed-4

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond” wakati akimuonesha moja ya tuzo kati ya  tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014. kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko.

unnamed-3

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond”  juu ya ushindi wake wa  tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014

unnamed-2 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na msanii Naseeb Abdul “Diamond”  alipomkaribisha Ikulu   kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014

unnamed-5

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea CD mpya ya msanii Naseeb Abdul “Diamond” baada ya kuoneshwa  tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014. 

unnamed-6

Tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda Naseeb Abdul “Diamond”  mwaka huu 2014

unnamed-9

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na msanii Naseeb Abdul “Diamond” baada ya kumkaribisha na  kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko, na kushoto ni katibu wa Bodi ya filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo

unnamed

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na msanii Naseeb Abdul “Diamond” alipomkaribisha ili  kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014

unnamed-8   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza  msanii Naseeb Abdul “Diamond” baada ya kumkaribisha na  kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014

unnamed-7

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa simu nma msanii Idris Sultani, mshindi wa shindano la mwaka huu la Televisheni la Big Brother Africa wakati alipokuwa na msanii Naseeb Abdul “Diamond” aliyemuonesha  tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014.