Daily Archives: January 11, 2015

MAREKEBISHO YA HOTUBA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika hafla ya kila  mwaka ambayo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huwaandalia Mabalozi wanaowakilisha nchi na Mashirika ya Kimataifa, ambayo ilifanyika  Ikulu tarehe 9 Jannuari, 2015, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitoa hotuba

Katika hotuba hiyo, Mheshimiwa Rais ameongelea mambo mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na yanayohusu mahusiano yetu ya kimataifa.

Pamoja na kuwa waandishi walikuwepo na kumsikia Rais akiongelea mambo hayo, ambayo pia tulituma hotuba yake kwenye vyombo vyote vya habari bado kuna upotoshwaji umefanyika katika suala muhimu linalohusu Tume ya Uchaguzi.

Hapa nanukuu kama Mhe. Rais alivyosema ambapo alitumia lugha ya Kingereza;

‘”The Electoral Commission is finalizing preparations for the referendum to be held on April 30th, 2015.We are doing everything within our powers to ensure that the problems identified in the pilot registration of voters exercise and others, are addressed speedily”.

Pilot study ambayo Kiswahili chake ni utafiti wa majaribio sehemu ndogo, ili kupata au kuangalia mambo mbalimbali na katika hili la Tume ya Uchaguzi ni pamoja na vifaa vinavyotumika kwa nia ya kurekebisha na kuboresha ili hatimaye utakapovitumia uwe na uhakika  katika eneo kubwa zaidi.

Ni kutokana na hiyo pilot study” ambapo Mheshimiwa ameiasa Tume ya Uchaguzi kufanyia kazi mapema iwezekanavyo marekebisho au maboresho katika mapungufu ambayo yameonekana ili hatimaye vifaa hivyo viweze kutumika kwa ufanisi zaidi. Hivyo,  hajapiga marufuku, wala kupinga au kusema vifaa hivyo havifai kwa matumizi.

Suala la majaribio ni suala la kawaida na la kitaalamu katika mambo mbalimbali na hata hili linalofanywa na Tume ya Uchaguzi sio jambo geni wala jipya kwa Tanzania.

Hivyo, nawaasa waandishi muwe waangalifu na mambo muhimu mnayoandika kwa sababu yanaigusa jamii , mkiwemo ninyi wenyewe.

Kwa hivyo ni muhimu kuyasoma na kuyaelewa na pale Mwandishi asipoelewa AMA kutatizwa na tafsiri ya jambo asione haya kuuliza kwani elimu haina mwisho

…….Mwisho……..

 

Imetolewa na;

Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,

Ikulu – Dar es Salaam.

11 Januari, 2015