Daily Archives: February 22, 2015

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKAGUA VIJIJI VILIVYOATHIRIWA NA MVUA ZA DHORUBA CHALINZE

RAIS KIKWETE AWAFARIJI WAHANGA WA DHORUBA CHALINZE ,BAGAMOYO.

 

Jumamosi 21,February, 2015.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana aliwafariji na kuahidi kuzisaidia kaya 40 ambazo nyumba zao ziliharibiwa vibaya na mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki iliyopita huko Chalinze,wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Katika ziara hiyo Rais Kikwete ambaye alikuwa amefuatana na mkewe mama Salma Kikwete alikagua Shule ya msingi Chalinze, Ofisi ya CCM, na nyumba kadhaa za wanakijiji ambazo ziliharibiwa vibaya na mvua hizo na kujeruhi baadhi ya wanavijiji walioangukiwa na nyumba zao.

“Nimepata taarifa ya maafa yaliyotokea, sikuwepo kwahiyo nimekuja kuwapa pole.Poleni sana Kwa wale ambao nyumba zimeharibika serikali inao utaratibu wa kusaidia.Mkurugenzi akipata taarifa atajua jinsi gani ya kuwasaidia.Lakini kuna misaada tunayoweza kutoa.Nasikia Mbunge ametoa msaada wa chakula na dawa pamoja na matibabu.Lakini Kwenye serikali tunao wajibu wetu.Mkurugenzi yupo taarifa zipilekwe kwake kwa uhakika ilitujue la kufanya.Poleni sana tutaendelea kusaidiana,” alisema Rais Kikwete ambaye pia ni Mkazi wa kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze.

Mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki liyopita iliharibu kabisa majengo nane katika kata ya Chalinze ambapo kuta zilibomoka mabati kuezuliwa na upepo mkali na miti kuangukia nyumba na kujeruhi wana kijiji kadhaa ambao walitibiwa katika hospitali ya Tumbi.Kaya 47 kutoka vijiji vya Msoga  na Tonga ziliathirika na mkasa huo. 2bdbdb

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwasili kwa helikopta katika kata ya Chalinze wakitokea jijini Dar es Salaam  February 21,2015  kukagua uharibifu ulioletwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kuharibu  makazi ya watu  na kujeruhi ambapo kaya 47 zikiathirika katika vijiji vya Msoga na Tonga

1bcvhb

 

 

3a

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  February 21,2015 aki kagua uharibifu ulioletwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kuharibu  makazi ya watu  na kujeruhi ambapo kaya 47 zikiathirika katika vijiji vya Msoga na Tonga

4

 

5

 

6

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wa kata Ya Chalinze wakikagua baadhi ya nyumba zilzoharibiwa vibaya baada ya kuangukiwa na miti kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika kata ya Chalinze na kuathiri kaya 47.Rais Kikwete alikagua uharibifu huo, kuzungumza na kuwafariji wana vijiji hao na kuahidi kuwasaidia katika janga hilo