Daily Archives: February 26, 2015

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AMTEMBELEA RAIS WA KWANZA WA ZAMBIA DKT. KENNETH KAUNDA NYUMBANI KWAKE LUSAKA ZAMBIA FEBRUARI 26,2015

1

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth Kaunda akimkaribisha nyumbani kwake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete huko kijijini kwake Mkango Barracks, State Lodge nje ya jiji la Lusaka leo Dkt. Kaunda ambaye alimwalika Rais Kikwete alifanya naye mazungumzo.

2

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la mke wa Rais wa Kwanza wa Zambia Mama Betty Mutinkhe Kaunda huko Mkango Barracks,State lodge, nje ya jiji la Lusaka 

3

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni nyumbani kwa Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth Kaunda(aliyesimama akiangalia) leo wakati alipomtembelea mwasisi wa taifa hilo.

4

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth David Kaunda nyumbani kwake  Mkango Barracks,State lodge, nje ya jiji la Lusaka 

5

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth Kaunda akimpa zawadi Rais Dkt.Jakaya Kikwete.

6

Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiagana na Rais wa Kwanza wa Zambia Mzee Kenneth Kaunda mara baada ya kumtembelea na kufanya naye mazungumzo 

7

RAIS LUNGU WA ZAMBIA AANDAA DHIFA KWA HESHIMA YA RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE FEBRUARI 25, 2015

1 - Copy

Rais  Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais wa Zambia Edgar Lungu pamoja na wake zao Mama Salma Kikwete na Mama Esther Lungu wakinyanyua glasi juu wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake ambao walifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Zambia.

3

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na Rais wa Kwanza wa taifa la Zambia Dkt.Kenneth Kaunda wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili nchini Zambia tayari amerejea jijini Dar es Salaam

unnamed

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Edgar Lungu wa Zambia wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia