Daily Archives: March 12, 2015

RAIS DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE AFARIJI WALIOPATWA NA MAAFA YA MVUA YA MAWE KATIKA KIJIJI CHA MWAKATA KAHAMA – SHINYANGA MACHI 12, 2015

1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Benson Mpesya juu ya madhara makubwa ya mali na maisha ya watu wakati wa ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

 5

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya makazi ya dharura kwa  familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

6

 

7

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa pole waalimu wa shule ya msingi ya Mwakata, wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, ambao pia ni waathirika wa  mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

  4

 

3

 

2msjjjc

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuwafariji waathirika wa Mvua ya Mawe,iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata,Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga,leo Machi 12,2015.

9

 

10

 

11

 

8

 Maelefu ya Wakazi wa Kahama wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia mara baada ya kutembelea na kujionea athari ya Mvua ya Mawe kwa wananchi wa Kijiji cha Mwakata,Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga,leo Machi 12,2015.

 

              TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Machi 12, 2015, amefanya ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

Rais Kikwete amewasili mjini Kahama kiasi cha saa nane mchana baada ya ndege yake kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi na kwa muda wa kiasi cha saa tatu ametembelea familia ambazo zimepata madhara makubwa zaidi kutokana na mvua hiyo iliyonyesha kwa kiasi cha saa moja tu kuanzia saa nne usiku Machi 3, mwaka huu, 2015 na kuambana na upepo mkali na mawe.

Watu 47 walipoteza maisha, 112 wakaumia, nyumba 657 zikabomolewa ama kuharibiwa na kaya 468 kuathirika katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata na tokea siku ya maafa, Serikali imetoa huduma za dharura za chakula, sehemu za kulala, huduma za afya na huduma nyingine muhimu kwa binadamu.

Baada ya kupatiwa maelezo ya kina na uongozi wa Mkoa wa Shinyanga chini ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali N. Lufunga, Rais Kikwete ameanzia ziara yake katika Kijiji cha Maghuhumwa, nyumbani kwa Bwana Masemba Maburi, ambaye alipoteza watoto watano katika maafa hayo. Rais Kikwete ametoa pole kwa wafiwa na kuzungumza na wananchi waliokuwepo kwenye msiba.

Bwana Maburi ambaye sasa anaishi katika nyumba ya jirani pamoja na familia yake na familia nyingine tatu amemweleza Rais Kikwete jinsi nyumba mbili ambako watoto hao na mama yao walipokuwa wamelala zilivyoanguka na mama huyo akalazimika kukimbilia nje kwa nia ya kutafuta msaada lakini watoto wakazidiwa na kupoteza maisha.

“Sijawahi kuona mvua kubwa, kali na yenye upepo mkali kiasi kile katika maisha yangu. Mvua ilianza saa nne usiku na ikanyesha kwa muda mfupi sana, nyumba zikaanguka ama kubomolewa. Jameni tusaidie kwa sababu tumekwazika,”Bwana Maburi amemwambia Rais Kikwete.

Baada ya kutoka katika Kijiji cha Maghuhumwa, Rais Kikwete amekwenda katika Kijiji cha Nhumbi ambako amempa pole Bwana Zacharia Limbe na familia yake ambayo ilipoteza wajukuu wanne katika maafa hayo ya mwanzoni mwa mwezi huu.

Akiwa nyumbani kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembea na kujionea makazi mapya ya dharura ya familia ambayo yamejengwa kwa msaada wa Serikali.

Baada ya kuondoka kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembelea eneo la makazi ya walimu wa Shule ya Msingi ya Mwakata, ambako walimu hao wamehifadhiwa katika fremu za maduka kutokana na athari za maafa hayo. Rais Kikwete amewapa pole walimu hao na kuwaambia: “Pole sana. Tuko pamoja. Tutaendelea kusaidiana kuona jinsi gani mnavyoweza kurejea katika maeneo yenu ya makazi ya kawaida.”

Rais Kikwete ataondoka kesho, Ijumaa, Machi 13, 2015, kurejea Dar es Salaam baada ya ziara hiyo maalum ya siku mbili katika Mkoa wa Shinyanga.

Ends

 

 

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

12 Machi, 2015

 

 

RAIS JAKAYA KIKWETE AAPISHA TUME YA UTUMISHI WA UMMA MACHI 12, 2015 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

1bfnvlfnvkl

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Wasita kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma muda mfupi baada ya Rais kuwaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam Machi 12, 2015 .kutoka kjushoto ni Bibi Salome Mollel (Kamishna)  Bibi Evelyne Itanisa (Kamishna) ,Bw. Mgeni Mwalimu Ally (Kamishna), Mwenyekiti wa Tume Dkt.Stephen James Bwana George Yambesi(Kamishna),Bwana Yahya Fadhili Mbila(Kamishna) na Bibi Adieu Nyondo(Kamishna)