Daily Archives: May 15, 2015

RAIS DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE KUONGOZA SHEREHE ZA KILELE CHA WIKI YA ELIMU KITAIFA MEI 15,2015 KATIKA UWANJA WA MICHEZO WA JAMHURI MJINI DODOMA

1

Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma  kuongoza sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa Mei 15,2015 

2

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na balozi wa jamhuri ya watu wan chi ya China Balozi  LU Youqin  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma  kwa ajili ya kuhudhuria kilele cha wiki ya Elimu kitaifa zilizofanyika kitaifa mkoani Dodoma Mei 15,2015 

3

 

4

 

5

Baadhi ya Wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali mjini Dodoma waliohudhuria sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15,2015 

1

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwanafunzi Agatha Julius Ninga kutoka Shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora akiwa ni miongoni mwa wanafunzi sita waliofaulu vizuri katika mitihani ya sayansi ya kidato cha nne mwaka jana 2014.Agatha alifanya vizuri katika somo la Biolojia.Rais Kikwete alitoa zawadi kwa wanafunzi, shule,halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri na kuongeza ufaulu katika mitihani ya Taifa kumaliza Elimu ya msingi na elimu ya sekondari.Tuzo na zawadi hizo zilitolewa leo katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya kilele cha  wiki ya elimu nchini.

2

 

D92A9276

Waziri wa Elimu Dkt.Shukuru Kawambwa akitoa tuzo  maalum mbili kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha  wiki ya elimu yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma 

3

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Elimu kitaifa iliyofanyika mjini Dodoma 

4

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wanafunzi Maria Sagasii na Neema Harry kutoka Shule ya msingi ya Ignatius ya mjini Dodoma wakionyesha viungo vya ndani vya mwili wa binadamu somo la Biolojia katia banda la maonyesho katika Uwanja wa michezi wa Jamhuri wa mjini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu 

RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AWATEMBELEA WATOTO WALIOFANYIWA UPASUAJI WA MOYO KATIKA HOSPITAL YA MUHIMBILI MEI 14, 2015

1

 

2

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Habiba Khalfan Lipande(6) ambaye amefanyiwa tiba ya kuziba tundu lililokuwa katika moyo wake kwa kutumia teknolojia mpya bila upasuaji wa kifua katika hospitali ya taifa Muhimbili.Mtoto Habiba kutoka katia kijiji cha Mavumba Mkoani Morogogoro ni mmoja kati wa watoto zaidi ya 70 watakofaidika na tiba ya moyo ikiwemo ya kuziba matundu bila ya upasuaji na ile ya kawaida ya upasuaji Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Kitengo cha Moyo inayoendeshwa kwa ufadhili ya shirika Al Muntada lenye makao yake makuu jijini London Uingereza na kufanya shughuli zake nyingi katika nchi ya Saudi Arabia.Rais Kikwete amewashukuru na kuwapongeza  madaktari hao  kwa kazi nzuri na kuwaomba kufanya zoezi hilo kuwa endelevu

1

 

2

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kisha kupiga picha ya pamoja na madaktari wa Shirika lisilo la kiserikali la Al Muntada lenye makao yake makuu jijini London Uingereza wanaoendesha zoezi la upasuaji na tiba ya moyo kwa zaidi ya watoto 70 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam