Daily Archives: June 18, 2015

KATIBU MKUU KIONGOZI AAGANA NA VIJANA ISHIRINI NA MOJA (21) WANAOKWENDA MAREKANI KWA MAFUNZO YA UONGOZI CHINI YA PROGRAMU YA RAIS BARACK OBAMA -YOUNG AFRICAN LEADERS INITIATIVE (YALI), IKULU, DAR ES SALAAM. 18 JUNI, 2015

1gfmfjn

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue tarehe 18 Juni, 2015 amekutana na vijana ishirini na moja (21) kutoka taasisi mbalimbali za umma na sekta binafsi wanaokwenda Marekani kujifunza masuala ya uongozi kwa kipindi cha wiki sita (06) Programu ya mafunzo hayo ijulikanayo kama The Mandela Washington Fellowship for Young African Leaders ilianzishwa na Rais Barack Obama wa Marekani mnamo mwaka 2010

2jhkhjkhk

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue 18 Juni, 2015 akiwa katika picha ya pamoja na vijana ishirini na moja (21) kutoka taasisi mbalimbali za umma na sekta binafsi wanaokwenda Marekani kujifunza masuala ya uongozi kwa kipindi cha wiki sita (06) Programu ya mafunzo hayo ijulikanayo kama ‘The Mandela Washington Fellowship for Young African Leaders’ ilianzishwa na Rais Barack Obama wa Marekani mnamo mwaka 2010

Thursday 18th June 2015

Chanzo :Ikulu

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue leo tarehe 18 Juni, 2015 amekutana na vijana ishirini na moja (21) kutoka taasisi mbalimbali za umma na sekta binafsi wanaokwenda Marekani kujifunza masuala ya uongozi kwa kipindi cha wiki sita (06).

Programu ya mafunzo hayo ijulikanayo kama ‘The Mandela Washington Fellowship for Young African Leaders’ ilianzishwa na Rais Barack Obama wa Marekani mnamo mwaka 2010 ili kuchangia ukuaji na uimarishaji wa misingi ya utawala bora, demokrasia, amani, ulinzi na usalama barani Afrika.

Balozi Sefue alitumia fursa hiyo kuwahimiza vijana kujitambua kuwa wao ni sehemu muhimu sana ya mabadiliko na mageuzi muhimu nchini na watumie fursa hiyo ya mafunzo kujifunza mbinu mpya, weledi, ujuzi na maarifa ili waje kuongoza mabadiliko na mageuzi yanayotakiwa nchini.

‘’Maendeleo ya nchi yetu yamo mikononi mwenu’’, alisisitiza. Balozi Sefue ameishukuru Serikali ya Marekani kwa msaada huu muhimu na akaeleza kuwa Serikali ya Tanzania inathamini sana mchango huo.

Aidha, Balozi Sefue alielezea jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha vijana wanapatiwa fursa za kujiendeleza ikiwa ni pamoja na kuongeza nafasi nyingi za elimu na ubora wa elimu yenyewe, kuboresha mitaala kwa kuingiza masuala ya ujasiriamali, ubunifu, mbinu za kujitegemea na kuanzisha utaratibu wa kuwawezesha vijana waliojumuika katika makundi.

Vile vile, Balozi Sefue aliwasihi vijana hao kwenda kuitangaza vizuri Tanzania na kuwezesha mtandao mpana zaidi wa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

Naibu Balozi wa Marekani nchini Bi. Virginia Blaser na maafisa wengine wa Ubalozi waliwasindikiza vijana hao ambao wameelezea furaha yao kubwa kwa kupata fursa hii adhimu.