Daily Archives: August 3, 2015

RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AREJEA NYUMBANI BAADA YA ZIARA RASMI YA KISERIKALI NCHINI AUSTRALIA AGOSTI 1,2015

1 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015 mara baada ya kurejea kutoka  Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove

2

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadik baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea  Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove  

3hkjnhknh Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine waliofika kumpokea alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  Agosti 1, 2015  akitokea  Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove.

1Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani Madabida  alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea  Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo  Mheshimiwa Peter Cosgrove

 

Akiwa nchini Australia Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot ambaye alimpongeza kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa  Katiba nchini Tanzania. 

Rais Kikwete pia alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove, kabla ya kukutana na wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania ambapo walizungumzia  namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika  kutokana na kupata gesi.

Tayari Serikali ya Australia na makampuni binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi stadi VETA na  tafiti mbalimbali katika Kilimo. 

Rais Kikwete alihitimisha ziara yake kwa kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla.