Daily Archives: August 8, 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA BARABARA YA NDUNDU-SOMANGA KILWA MKOANI LINDI AGOSTI 7, 2015

3

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli(wapili kushoto),Balozi wa Kuwaiti nchini Tanzania Mhe.Jassem Ibrahim Al Najem(kulia) pamoja na mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait Bwana Abdulrahman Al Hashim(wapili kulia) wakifunua kitambaa katika jiwe kuashiria kufungua rasmi barabara ya kilometa 60 ya Ndundu-Somanga wakati wa hafla ikiyofanyika katika kijiji cha Marendego Wilaya ya Kilwa leo.Barabara hiyo imefadhiliwa na mfuko wa Kuwait. 

4Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Mwakirishi wa Mfuko wa Kuwaiti Bwana Abdurahman Al Hashim, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe.Jassem Ibrahim Al Najem wakikata utepe kufungua rasmi Barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilomita 60 katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Marendego Wilaya ya Kilwa.Barabara hiyo imejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Kuwaiti.Wengine katika picha ni  mkuu wa mkoa wa Lindi Mwantum Mahiza,Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.  

2Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa sherehe ya ufunguzi wa Barabara ya Ndundu Somanga 

1Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mwakilishi wa mfuko wa Kuwait Bwana Abdulrahman Al Hashim wakati wa sherehe ya ufunguzi wa Barabara ya Ndundu-Somanga iliyofadhiliwa na mfuko huo.Kulia ni Balozi wa Kuwaiti nchini Tanzania Mhe.Jassem Ibrahim al Najem 6Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalamiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe ya ufunguzi wa Barabara ya Ndundu Somanga

RAIS KIKWETE AZINDUA RASMI BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA (TADB) AGOSTI 07,2015

1

 

2

 

3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wadau wa kilimo na taasisi za fedha wakati akizindua rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam

4

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akizindua rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam

5

Vifijo baada ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua  rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam 

6

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo, Mhe Stephen Wasira, Waziri wa Fedha Mhe Saada Mkuya na viongozi na watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam  

7

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo, Mhe Stephen Wasira, Waziri wa Fedha Mhe Saada Mkuya, Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mkurugenzi Mkuu wa TIB Bank Bw. Peter Noni  na viongozi na watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam   

 

 

8Msanii akiburudisha kwa ngoma kutoka Zanzibar baada ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua  rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam