Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuzindua rasmi kivuko cha MV.Mafanikio huko eneo la Msangamkuu mjini Mtwara
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli na viongozi waandamizi serikalini wakikata utepe kuzindua rasmi kivuko MV Mafanikio huko Msangamkuu Mkoani Mtwara Agosti 9,2015
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama mara baada ya kuwasili Mkoani Mtwara leo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete aikiwa ndani ya kivuko cha MV.Mafanikio mara baada ya kukifungua kivuko hicho ambacho kinafanya safari zake kati ya Mtwara Mjini hadi Msangamkuu Agosti 9,2015
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na ujumbe wake akishuka ndani ya kivuko cha MV.Mafanikio mara baada ya kuwasili eneo la Msangamkuu Agosti 9,2015 kwa ajili ya kuhutubia wananchi ya wa kata ya Msangamkuu Mtwara
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la Taifa NHC Nehemia Mchechu akimweleza jambo Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za NHC eneo la shangani Mjini Mtwara leo jioni
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa TAMISEMI Hawa Ghasia aliyemwakilisha Waziri wa Ardhi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Bwana Nehemia Mchechu Wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua rasmi mradi wa ujenzi wa nyumba za NHC eneo la Shangani Mtwara.Wapili kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete na wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bibi Halima Dendego.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi tawi la Benki Kuu mjini Mtwara Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu Dkt.Benno Ndulu na kulia ni Naibu Waziri wa Fedha Bwana Mwigulu Nchemba