Daily Archives: September 8, 2015

RAIS KIKWETE APOKEA TUZO YA KIONGOZI BORA AFRIKA MASHARIKI IKULU DAR ES SALAAM SEPTEMBA 8,2015

awwwe

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  amepokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki kutoka katika taasisi ya East Africa Book of Records yenye makao yake makuu jijini Kampala Uganda.Pichani kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt.Paul Bamutize akimkabidhi Rais Kikwete tuzo hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam September 08,2015  1

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kumbukumbu maalum ya taasisi ya East Africa Books of Records mara baada ya kupokea tuzo maalum ya kiongozi bora Afrika mashariki kwa kudumisha amani nchini na katika jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla hususan Kenya baada ya uchaguzu mkuu na Burundi hivi karibuni.Kushoto akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Africa Book of Records Dkt.Paul Bamutize na kulia ni Mkuu wa kitengo cha utafiti katika taasisi hiyo Bwana Luzindana Adam Buyinza.  

2

Baadhi ya Wageni walihudhuria hafla hiyo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

3

Mwakilishi kutoka ubalozi wa Uganda nchini Tanzania Bwana Stephen Kiyingi akitoa hotuba yake na ushuhuda jinsi Tanzania ilivyopiga hatua kubwa ya maendeleo katika miaka kumi iliyopita.

4

Rais Dkt.Jakaya Mrisho akitoa hotuba yake baada ya kupokea Tuzo ya Kingozi bora Afrika Mashariki.  

8

Wataalamu wa Utafiti kutoka Taasisi ya East Africa Book Of Records wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada kutunikiwa Tuzo hiyo.Kutoka kjushoto ni Kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt.Paul Bamutize,Watatu kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Utafili cha taasisi hiyo Bwana Luzindana  Adam Buyinza na kulia ni Afisa mwandamizi wa Taasisi hiyo Bwana Kato Issa

 6

 

 Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, mabalozi kutoka nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tassisi ya East Africa Book of Records ikulu jijini Dar es Salaam leo.

 

7

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza mabalozi kutoka nchi za Afrika ya Mashariki muda mfupi baada ya kupokea Tuzo

 

 

RAIS KIKWETE AWAPA POLE MAJERUHI YA MSONGAMANO WA WANANCHI BAADA YA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO JANA SEPTEMBER 07,2015

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa Morogoro Ndg. Hassan Bantu alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.

 Mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo

 Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo

 Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi Flora Maduka akiwa kitandani pake hospitalini hapo baad ya kujeruhiwa katika msongamano huo

 Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi. Jalia Mohamed akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo

 Rais Kikwete akiendelea kutoa pole kwa majeruhi

 “Pole sana….” Rais Kikwete akimfariji mmoja wa majeruhi

 

 Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyeungua kwa moto

  Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyevunjika mguu wakati akicheza kwenye mti

Rais Kikwete akimpa pole mvulana ambaye aligongwa na gari wakati akielekea kumsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana 

Rais Kikwete alipata fursa ya kutembelea wodi ya watoto na kuwapa pole kwa kuumwa kwao

Rais Kikwete akiongea na wanafunzi waliokuwepo hospitalini hapo kumtembelea mgonjwa

Rais Kikwete alizongwa na wananchi waliokuwa na hamu ya kuongea naye 

Rais Kikwete akitoa mapendekezo ya kupanua hospitali hiyo ambayo ina eneo kubwa lakini majengo machache ya chini. Alipendekeza uongozi wa hospitali na mkoa ubuni namna ya kuipanua kwa kujenga majengo ya ghorofa ili kuwepo na wodi na sehemu nyingi zaidi za huduma.

Mwishoni Rais Kikwete aliongea na wanahabari wa kutoka vyombo mbalimbali na kueleza masikitiko yake kwa yaliyotokea jana Uwanja wa Jamhuri baada ya mkutano wa kampeni kumalizika.

Rais Jakaya Kikwete akiongea na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya baada ya kuwajulia hali majeruhi wa msongamano baada ya mkutano wa kampeni uwanja wa Jamhuri Morogoro jana