Daily Archives: October 9, 2015

RAIS JAKA MRISHO KIKWETE ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA AKIWA NA WAJUKUU


Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe za miaka 65 ya kuzaliwa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na miaka 55 ya kuzaliwa mdogo wake Yusufu Mrisho Kikwete jana jioni jijini Dar es salaam. Rais Kikwete na mdogo wake walisherehekea siku zao za kuzaliwa kwa kukata na kula keki na wajukuu wao na wa jamaa, ndugu na marafiki waliowaalikwa kwenye sherehe hii fupi iliyojaa furaha na bashasha.

Keki

Wajukuu wakimchukua babu wakamwimbie na kukata naye keki

Mjukuu akiogoza wajukuu wenzie kumwimbia babu

Wajukuu wakimwimbia babu

Wajukuu wakimsaidia babu kupuliza mishumaa

Babu akikata keki huku wajukuu wakiisubiri kwa hamu

Wajukuu wakiendelea kusubiri keki

Babu akiwalisha wajukuu keki

Kila mjukuu alipata keki

Keki ya babu taaamuu…..

Mufti Mkuu wa Taanzania na wageni wengine waalikwa wakishuhudia babu akiwalisha keki wajukuu

Sasa ni zamu ya babu kulishwa keki na wajukuu  

Babu akiendelea kulisha keki wajukuu

Bibi, Mama Salma Kikwete, akimsaidia Babu kuhakikisha kila mjukuu kapata keki

Kila mjukuu anapata keki

Babu na bibi wakiendelea kuandaa keki

Selfie zilikuwepo pia