Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa Wimbo wa Taifa katika kilele cha Sherehe za kutimiza Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar Januari 12,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia mamia ya wananchi (hawapo pichani) katika kilele cha Sherehe za kutimiza Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifuatilia kwa makini matukio mbalimbali katika kilele cha Sherehe hizo za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika uwanja wa Aman.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika Sherehe hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakiangalia gwaride la heshima lililokuwa likipita mbele yao katika kilele cha Sherehe za kutimiza Miaka 52 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama vikitoa heshima mbele ya Mgeni Rasmi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka kwenye Uwanja wa Aman, Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Aman, Zanzibar.