Monthly Archives: April 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI LEO TAREHE 25 APRILI, 2016 AMEFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 25 YA TANZANIA BARA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 25 ya Tanzania Bara. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa.  Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

  1. Arusha –                     Richard Kwitega
  2. Geita –                         Selestine Muhochi Gesimba
  3. Kagera –                      Armatus C. Msole
  4. Kilimanjaro –            Eng. Aisha Amour
  5. Pwani –                       Zuberi Mhina Samataba
  6. Shinyanga –                Albert Gabriel Msovela
  7. Singida –                     Dr. Angelina Mageni Lutambi
  8. Simiyu –                      Jumanne Abdallah Sagini
  9. Tabora –                     Dkt. Thea Medard Ntara
  10. Tanga –                       Eng. Zena Said

Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo;

  1. Kigoma –                     Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita)
  2. Morogoro –                Dkt. John S. Ndunguru (Kutoka Mkoa wa Kigoma)

Makatibu Tawala waliobakishwa katika vituo vyao vya sasa vya kazi ni kama ifuatavyo;

  1. Dar es salaam –         Theresia Louis Mbando
  2. Dodoma –                  Rehema Hussein Madenge
  3. Iringa –                        Wamoja Ayubu Dickolagwa
  4. Katavi –                       CP Paul Chagonja
  5. Lindi –                         Ramadhan Habibu Kaswa
  6. Mara –                        Benedict Richard Ole Kuyan
  7. Manyara –                  Eliakimu Chacha Maswi
  8. Mbeya-                       Mariam Amri Mjunguja
  9. Mtwara –                     Alfred Cosmas Luanda
  10. Mwanza –                   CP. Clodwing Mathew Mtweve
  11. Njombe –                    Jackson Lesika Saitabau
  12. Rukwa –                      Symthies Emmanuel Pangisa
  13. Ruvuma –                    Hassan Mpali Bendeyeko

Makatibu Tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili, 2016 saa tatu asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,

IKULU Dar es salaam

25 Aprili, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WATATU KUTOKA NCHI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM APRIL 22,2019

1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake Francisco Montecillo Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Vatican alifika Ikulu kwa ajili ya kuagana na Rais Dkt. Magufuli mara baada ya kumaliza muda wake ya Ubalozi nchini.

2ssfgfs 

3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake nchini Francisco Montecillo

5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake Francisco Montecillo Ikulu jijini Dar es Salaam

4eqeqeBalozi wa Algeria hapa nchini Belabed Saada akikabidhi ujumbe uliotoka kwa Rais wa Algeria kuja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

6Balozi wa Algeria hapa nchini Belabed Saada akikabidhi ujumbe uliotoka kwa Rais wa Algeria kuja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

8hdhjdhRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam

7 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque wapili kutoka kulia pamoja na waakilishi wengine wa Serikali pamoja na Ubalozi wa Canada.