Daily Archives: April 7, 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AREJEA NYUMBANI APRIL 7,2016 KUTOKA NCHINI RWANDA IKIWA NI SAFARI YAKE YA KWANZA NJE YA NCHI TANGU ACHAGULIWE KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili April 7, 2016. 

3 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 

4 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange huku Inspekta jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu akisubiri zamu yake  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili April 7, 2016

5 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Msajili wa vyama vya Siasa Mhe Jaji Francis Mutungi mara baada ya kutua  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili  April 7, 2016. 

6 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili April 7, 2016. 

7

 

8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje, Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili  April 7, 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI SHUGHULI ZA KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA KIMBARI (KWIBUKA) KIGALI NCHINI RWANDA APRIL 7, 2016

1

 

2 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali mbele ya makaburi ya watu waliouwawa katika Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Kulia ni Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na Mkewe Janeth Kagame na mtoto.

3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwasha mwenge wa matumaini kuashiria kutotokea tena kwa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda.

4 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, mama Janeth Magufuli, Mama Janeth Kagame wakisikiliza historia ya jinsi mauaji ya kimbari yalivyotokea katika eneo la kumbukumbu ya mauji hayo.

5 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, mama Janeth Magufuli, Mama Janeth Kagame waiwa wamesimama kutoa heshima kwa watu waliofariki katika mauaji hayo ya kimbari.

6Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiangalia kwa uchungu mafuvu ya watu waliopoteza maisha katika mauaji hayo ya kimbari.

7 Wageni mbalimbali waliofika kwenye kumbukumbu hizo.

8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha za watoto waliouwawa kinyama katika eneo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbaria Gishozi Kigali nchini Rwaanda

10Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kitabu chenye maelezo mbalimbali kuhusu mauaji hayo ya kimbari.

12 Rais wa Rwanda Paul Kagame akimpokea Rais Magufuli katika viwanja vya Gishozi kabla ya kwenda kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya watu waliouwawa katika mauaji ya Kimbari.

13Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na Rais Magufuli pamoja na Mama Janeth Magufuli, Janeth Kagame wakielekea kwenye makaburi ya halaiki katika makumbusho ya mauaji ya Kimbari, Gishozi Kigali nchini Rwanda.