Monthly Archives: January 2017

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA KUTANGAZA JINA RASMI LA KITUO CHA AMANI NA USALAMA KILICHOPEWA JINA LA MWALIMU JULIUS NYERERE KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRICA (AU) ADDIS ABABA NCHINI ETHIOPIA JANUARI 29,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa Mataifa mbalimbali hawapo (pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na Usalama kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Abba nchini Ethiopia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi wa mataifa mabalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika jengo jipya la kituo cha Amani na Usalama (JULIUS NYERERE) lililopo katika Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa nchini Ethiopia. Januari 29,2019

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AELEKEA ADDIS ABABA, ETHIOPIA, KWENYE MKUTANO WA 28 WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA JANUARI 28,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Mungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Januari 28, 2017 tayari kwa safari ya Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU). Rais Assoumani alikuwa akitokea Comoro kupitia Dar es salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Comoro nchini   Dk.Ahamada El Badaoui Mohamed  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa  Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kwenda  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).