Daily Archives: February 18, 2017

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AMJULIA HALI WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA DAVID MSUYA NYUMBANI KWAKE UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM FEBRUARI 18,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam alipokwenda kumjulia hali, Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alikuwa ametoka hospitalini alipokuwa amelazwa mara baada ya hali yake kuwa nzuri na kuruhusiwa na kurejea nyumbani Februari 18,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nyumbani kwake jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

 

Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimsindikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifika nyumbani kwake kumjulia hali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.

AMIRI JESHI MKUU NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI KUNDI LA 60/16 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM FEBRUARI 18,2017

 

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 60/16 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  Februari 18, 2017 

 

 

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride la heshima linaloundwa na Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 60/16 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  Februari 18,2017

 

 

 

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwapa zawadi wanafunzi maafisa waliofanya vizuri katika masomo ya darasani na vitendo wakatia alipokua akitunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 60/16 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  Februari 18, 2017

 

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati  ya  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 60/16 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Februari 18, 2017

 

 

Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 60/16 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  wakivalishana vyeo baada ya kupewa kamshini na Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  Februari 18, 2017

 

 

Gwaride la Maafisa wa Kundi la 60/16 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) likitoka uwanjani baada ya kupewa kamshini na Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  Februari 18, 2017

 

 

 

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali wakiangalia kikundi cha ngoma cha Jeshi wa wananchi wa Tanzania baada ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 60 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Februari 18,2017

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Makamo wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa  na viongozi wa juu wa jeshi la ulinzi na wizara ya ulinzi katika picha ya pamoja na asikali maafisa waliotunukiwa kamisheni Kundi la 60/16 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Februari 18,2017