Daily Archives: March 6, 2017

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA UWANJA WA NDEGEVITA WA KAMBI YA NGERENGERE, MOROGORO MACHI 6,2017

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli akijiandaa kufyatua risasi ya bastola kuashiria matumizi rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere mkoani Morogoro  Machi 6, 2017

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli na Balozi wa China nchini Dkt katika picha ya pamoja na viiongozi mbalimbali baada ya uzinduzi  rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa  Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017.

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli na Balozi wa China nchini Dkt wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi  rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere mkoani Morogoro Machi 6, 2017

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa  uzinduzi  rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa  Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017.

 

 

UTEKELEZAJI WA AHADI ZA MH. RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ALIZOZITOA KATIKA ZIARA YAKE YA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mara baada ya mahubiri katika Kanisa hilo. Rais Dkt. Magufuli amechangia Kanisa hilo Mifuko 200 ya Saruji kwa ajili ya kuendeleza kazi ya ujenzi wa uzio Kanisani hapo

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia Waumini wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara mara baada ya mahubiri.

Kaimu Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mifuko 200 ya Saruji ili kutimiza Ahadi ya Rais aliyoitoa kanisani hapo March 5,2017

Kaimu Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi fedha kiasi cha Shilingi Milioni 35 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ili kutekeleza ahadi aliyoitoa Rais wakati alipopita katika Kijiji cha Somanga na Mnonela. Katika kijiji cha Somanga Rais Dkt. Magufuli aliahidi kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 20, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya na kwa upande wa Mnonela aliahidi kiasi cha Shilingi milioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Afya .

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akisaini kuthibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha ambazo ni utekelezaji wa Ahadi za Rais Dkt. Magufuli wakati alipofanya ziara mkoani humo

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kituo cha Afya mnonela katika Jimbo la Mtama ambapo aliahidi kuchangia kiasi cha fedha Shilingi Milioni 15 ambazo tayari Mkuu wa Mkoa wa Lindi ameshakabidhiwa