Daily Archives: July 17, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBEMAGUFULI AWAANDALIA DHIFA YA KITAIFA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA VYA AFRIKA PAMOJA NA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) WANAOSHIRIKI KATIKA MKUTANO HUO WA VIONGOZI JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wakati wa dhifa ya Kitaifa aliyowaandalia Viongozi wote wanaoshiriki Mkutano huo jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika Dhifa ya kitaifa aliyowaandalia viongozi wa vyama vya siasa kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja na Chama cha Kikomunisti cha China cha CPC Ikulu jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa vyama vya siasa kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja na Chama cha Kikomunisti cha China cha CPC wakiwa katika Dhifa hio ya kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wakiangalia burudani kutoka katika kikundi cha TOT katika Dhifa hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika hafla hiyo ya chakula cha jioni.

Kikundi cha TOT kikitumbuiza katika Dhifa ya kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya hafla hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya Dhifa ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO KATI YA VYAMA VYA SIASA VYA AFRIKA NA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) JIJINI DAR ES SALAAM.JULAI 17,2018

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika kabla ya kufungua mkutano kati ya viongozi wa vyama hivyo na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika mkutano huo wa viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika na Chama hicho cha CPC jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bashiru Ally akihutubia katika mkutano huo.

 

Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

 

Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam.