Daily Archives: July 26, 2018

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA MPANGO WA CHAKULA DUNIANI (WFP) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.JULAI 26,2018.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley zawadi ya Picha ya moja ya mbuga za wanyama zilizopo nchini pamoja na kinyago cha mpingo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael Dunford mara baada ya mazungumzo na ujumbe huo wa Shirika hilo la kimataifa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi wa kanda wa (WFP) Bi. Lola Castro mara baada ya mazungumzo na ujumbe huo wa Shirika hilo la kimatifa Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael Dunford pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga wakishuhudia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga mara baada mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley wanne kutoka (kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga watatu kutoka kulia, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Omary Mgumba wapili kutoka kulia, Balozi Zuhura Bundala wakwanza kushoto akifatiwa na na Mkurugenzi wa kanda wa (WFP) Bi. Lola Castro pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael Dunford watatu kutoka kushoto.