Daily Archives: August 21, 2018

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA CHATO KATIKA MAZISHI YA DADA YAKE MAREHEMU MONICA MAGUFULI YALIYOFANYIKA CHATO MKOANI GEITA.AGOSTI 21,2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsaidia Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakuweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Monica Joseph Magufuli likipelekwa Kanisani kwa ajili ya Misa takatifu Chato Mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kanisani katika Misa takatifu ya kumuombea Marehemu Dada yake Monica Magufuli. Wengine katika picha ni Mama yake Suzana Magufuli, Stanslaus Lori Madulu(Mme wa marehemu) , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na viongozi mbalimbali wa Kiserikali.

Baba Askofu mkuu Mwandamizi  Yuda Thaddeus Ruwaichi akiongoza Misa ya kumuombea Marehemu Monica Magufuli Chato mkoani Geita

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkewe Mama Marry Majaliwa wakitoa heshma zao za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Baba Askofu mkuu Mwandamizi  Yuda Thaddeus Ruwaichi akiongoza Misa ya kumuombea Marehemu Monica Magufuli Chato mkoani Geita

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo ndani ya kaburi la Monica Joseph Magufuli wakati wa mazishi yaliyofanyika katika kijijini cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la Dada yake Monica Magufuli mara baada ya mazishi.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la Monica Magufuli wakati wa Mazishi katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga wakati shuguli za mazishi zikiendelea katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akitoa heshma za Mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anazungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kumaliza mazishi ya Dada yake Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.