Monthly Archives: September 2018

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MJUKUU WA MALKIA ELIZABETH II WA UINGEREZA PRINCE WILLIAM IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.SEPTEMBA 27,2018

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William aliyeambatana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke pamoja na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William picha ya wanyama wanaopatikana katika mbuga mbalimbali nchini mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William Kamusi ya Kiswahili mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Picha kutoka kwa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha hiyo inamuonesha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa anazungumza na Malkia wa Uingereza Elizabeth II 

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUFUA UMEME WA STIEGLER”S GORGE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.SEPTEMBA 24,2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi waandamizi wa serikali wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler’s Gorge wakisimama kwa dakika kadhaa kuwakumbuka marehemu waliopoteza masiha kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere huko Ukara wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza majuzi. Hii ilikuwa ni kabla ya kuanza kwa kikao kazi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam.Septemba 24, 2018.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi waandamizi wa serikali wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler’s Gorge pamoja na wataalamu wakati wa  kikao kazi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam.Septemba 24, 2018.