Daily Archives: September 7, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA MTO MARA LENYE UREFU WA MITA 94 LINALOUNGANISHA KATI SERENGETI NA TARIME PIA AHUTUBIA WANANCHI WA NYAMONGO MKOANI MARA.SEPTEMBA 7,2018

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tarime mjini mara baada ya kuwasili akitokea katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

 

 

Kwaya ya Chuo cha Ualimu Tarime ikitoa burudani mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili Tarime mjini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanakwaya ya Chuo cha Ualimu Tarime mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano Tarime mjini.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Tarime mjini mara bada ya kuwahutubia.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Nyamongo mkoani Mara wakati akitokea Mugumu Serengeti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Nyamongo mkoani Mara wakati akitokea Mugumu Serengeti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Sekondary Ingwe iliyopo Nyamongo Wilayani Tarime Monica Benard kiasi cha Shilingi milioni tano kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya shule hiyo kutokana na vipaumbele vyao.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ingwe ya Nyamongo Tarime mkoani Mara Monica Benard akionesha kiasi cha Shilingi milioni tano alizokabidhiwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya maendeleo ya shule yao. Pia Rais Dkt. Magufuli aliendesha Harambee ya papo kwa hapo ambapo zilipatikana jumla ya Shilingi milioni 26 kwa ajili ya maendeleo ya Shule hiyo.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyansura Serengeti mara baada ya kukagua mradi wa daraja la mto mara lenye urefu wa mita 94 linalounganisha katika ya Wilaya ya Serengeti na Tarime mkoani Mara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua daraja hilo la mto mara lenye urefu wa mita 94 linalounganisha katika ya Wilaya ya Serengeti na Tarime mkoani Mara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Nyambura Nyamarasa ambaye alikuwa na kero ya kulishiwa na shamba lake na mfugaji mmoja huko Mugumu Serengeti mkoani Mara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa shilingi milioni moja Nyambura Nyamarasa ambaye alikuwa na kero ya kulishiwa na shamba lake na mfugaji mmoja huko Mugumu Serengeti mkoani Mara.

 

Sehemu ya Daraja la mto mara mita 94 ambalo ujenzi wake unaendelea na litaunganisha kati ya katika ya Wilaya ya Serengeti na Tarime mkoani Mara.