Monthly Archives: November 2018

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WAHUDHURIA MISA YA SHUKURANI YA UHAI YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA KUTIMIZA UMRI WA MIAKA 80

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimpa zawadi ya kadi na kisha kumpongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa na mkewe Mama Anna Mkapa kwa kutimiza umri wa miaka 80 katika Misa ya Shukurani ya uhai iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam. Novemba 12, 2018

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa pamoja na Maaskofu wakati wa Misa ya Shukrani kwa Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam.Novemba 12, 2018

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea kwa furaha na  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa baada ya  Misa ya Shukurani kwa  Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata  jijini Dar es salaam.Novemba 12, 2018

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Misa ya Shukurani ya  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam.Novemba 12, 2018.Kulia kwa Mhe. Mkapa ni mkewe Mama Anna Mkapa

RAIS DKT. JOHN PIMBE MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI SABA (7) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.NOVEMBA 12,2018

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwaapisha Viongozi saba wakiwemo Mawaziri wawili, Naibu Mawaziri wanne, pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwaapisha Viongozi saba wakiwemo Mawaziri wawili, Naibu Mawaziri wanne, pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwaapisha Viongozi saba wakiwemo Mawaziri wawili, Naibu Mawaziri wanne, pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Viongozi mbalimbali waliopishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakila Kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kulia ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu, Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashugwa, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mwita Waitara pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msofe.

Viongozi mbalimbali waliopishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakisaini Hati za viapo vyao vya Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda pamoja na Waziri wa zamani wa Wizara hiyo Charles Mwijage mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Aboubakary Zebeiry mara baada ya hafla ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ngugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Kamishna wa Maadili Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela pamoja na Viongozi mbalimbali waliopishwa pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mwita Waitara kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Joseph Kakunda kuwa Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Constantine Kanyasu kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Japhet Ngailonga Hasunga kuwa Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma wakishuhudia tukio hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari waliofika Ikulu kwa ajili ya kutangaza tuko la Uapisho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Innocent Bashugwa Naibu Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma wakishuhudia tukio hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Mstaafu January Msofe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msofe mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.