Monthly Archives: March 2019

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KUKAGUA KAZI YA UPAKAJI WA RANGI NDEGE YA FOKER 50 ILIYOKUWA IKITUMIWA KUBEBA VIONGOZI AMBAYO ITAANZA KUBEBA ABIRIA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mhandisi Julius Ndyamukama wakwanza (kushoto) pamoja na Richard Mayongela watatu kutoka (kushoto) ambaye uteuzi wake ulitenguliwa hivi karibuni wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kukagua kazi ya upakaji wa rangi katika ndege aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali ambayo sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali na sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Rais Dkt. Magufuli alizuia ndege hiyo kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kazi hiyo ambapo ingegharimu zaidi ya Shilingi milioni 160 wakati kazi hiyo imefanywa na mafundi wa ndani kwa gharama ya shilingi miloni 7.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya ndani ya ndege hiyo ambapo ufungaji wa viti vipya umekamilika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka katika ndege hiyo aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali na sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wafanyakazi mbalimbali wa Shirika la ndege la Air Tanzania hawapo pichani wakati akitoka kufanya ukaguzi wa kazi ya upakaji rangi pamoja na uwekaji wa viti vipya katika ndege hiyo aina ya Foker 50.

Sehemu ya ndani ya Ndege hiyo ya Foker 50 ambayo kazi ya ufungaji wa viti vipya kutoka 32-48 umekamilika na kazi ya upakaji wa rangi ikielekea ukingoni. Hapo awali ndege hiyo ilikuwa iende nje ya nchi kwa ajili ya kupaka rangi na kuchora ndembo ya twiga kwa gharama zaidi ya Shilingi milioni 160 kabla ya Rais Dkt. Magufuli kutoa maagizo kazi hiyo ifanyike nchini na mafundi wa ATCL ambapo gharama yake ni Shilingi miloni 7.

Sehemu ya n je ya Ndege hiyo ya Foker 50 ambayo kazi ya ufungaji wa viti vipya kutoka 32-48 umekamilika na kazi ya upakaji wa rangi ikielekea ukingoni. Hapo awali ndege hiyo ilikuwa iende nje ya nchi kwa ajili ya kupaka rangi na kuchora ndembo ya twiga kwa gharama zaidi ya Shilingi milioni 160 kabla ya Rais Dkt. Magufuli kutoa maagizo kazi hiyo ifanyike nchini na mafundi wa ATCL ambapo gharama yake ni Shilingi miloni 7.

Sehemu ya n je ya Ndege hiyo ya Foker 50 ambayo kazi ya ufungaji wa viti vipya kutoka 32-48 umekamilika na kazi ya upakaji wa rangi ikielekea ukingoni. Hapo awali ndege hiyo ilikuwa iende nje ya nchi kwa ajili ya kupaka rangi na kuchora ndembo ya twiga kwa gharama zaidi ya Shilingi milioni 160 kabla ya Rais Dkt. Magufuli kutoa maagizo kazi hiyo ifanyike nchini na mafundi wa ATCL ambapo gharama yake ni Shilingi miloni 7.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali na sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Rais Dkt. Magufuli alizuia ndege hiyo kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kazi hiyo ambapo ingegharimu zaidi ya Shilingi milioni 160 wakati kazi hiyo imefanywa na mafundi wa ndani kwa gharama ya shilingi miloni 7.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mafundi wazalendo ambao wamefanya kazi ya kuandika na kuchora nembo ya Twiga pamoja na kupaka rangi ndege hiyo ya Foker 50 kwa gharama ya Shilingi milioni 7. Pia Rais Dkt. Magufuli amewazawadia mafundi hao kiasi cha Shilingi milioni 10 kutokana na kazi yao nzuri ya kizalendo walioifanya. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi wa ATCL Ladislaus Matindi wakati wa Ukaguzi wa ndege hiyo aina ya Foker 50

 Sehemu ya Ndani nan je ya Ndege hiyo ya Foker 50 ambayo kazi ya ufungaji wa viti vipya kutoka 32-48 umekamilika na kazi ya upakaji wa rangi ikielekea ukingoni. Hapo awali ndege hiyo ilikuwa iende nje ya nchi kwa ajili ya kupaka rangi na kuchora ndembo ya twiga kwa gharama zaidi ya Shilingi milioni 160 kabla ya Rais Dkt. Magufuli kutoa maagizo kazi hiyo ifanyike nchini na mafundi wa ATCL ambapo gharama yake ni Shilingi miloni 7.

RAIS MHE. DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA MPIRA WA MIGUU TAIFA STARS NA BONDIA HASSAN MWAKINYO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars ambao walifika Ikulu mara baada ya kufanikiwa kufuzu kushiriki Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes magoli 3-0 jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Rais wa TFF Walace Karia, Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo wapili kutoka kushoto katika picha ya pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars ambao walifika Ikulu mara baada ya kufanikiwa kufuzu kushiriki Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes magoli 3-0 jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakionesha ishara ya magoli matatu ambayo timu ya Taifa iliupata siku ya jumapili zidi ya Timu ya Taifa ya Uganda The Craines na kufanikiwa kufuzu kucheza Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON nchini Misri baadae mwaka huu.

Sehemu ya Wachezaji wa wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mchezaji wa Timu ya Taifa Taifa Stars Shabani Iddi Chilunda mara baada ya kumaliza kuzungumza na wachezaji hao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji ya Timu ya Taifa Stars ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wanne kutoka kushoto waliokaa pamoja na wachezaji Wachezaji wa wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Ikulu jijini Dar es Salaam.

Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo kutoka Tanga akijitambulisha Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza kuhusiana na mafanikio yake makubwa aliyoyapata katika ngumi za kulipwa pamoja na kuitangaza nchi kimataifa.

Mfungaji wa goli la pila la Taifa Stars zidi ya Uganda Erasto Nyoni akijitambulisha Ikulu jijini Dar es Salaam.

Bondia wa Ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo kutoka Tanga akizungumza mara baada ya kupewa nafasi Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Bondia Hassan Mwakinyo alipokuwa akizungumza.

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Jonas Mkude akifurahia jambo wakati wakiwa Ikulu jijini Dar es Salaam pamoja na wachezaji wenzake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kocha wa Taifa Stars Emanuel Amunike mara baada ya kumaliza kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Peter Tino ambaye alifunga goli moja lililoipeleka Tanzania kwa mara ya kwanza katika michuano ya AFCON mwaka 1980 iliyofanyika nchini Nigeria. Pia Rais Dkt. Magufuli amemsaidia mchezaji huyo wa zamani kiasi cha Shilingi milioni tano.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anapata chakula cha mchana na viongozi pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Ikulu jijini Dar es Salaam