Daily Archives: May 29, 2019

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWEKA SHADA LA MAUA KATIKA MAKABURI YA MASHUJAA WA ZIMBABWE KATIKA ENEO LA NATIONAL HEROES ACRE WEST WING HARARE NCHINI HUMO. MEI 29,2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa mbele ya mnara wa Kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa wa Taifa la Zimbabwe kabla ya kuweka shada la maua katika eneo hilo lililopo kilometa saba kutoka jiji la Harare nchini Zimbabwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua mbele ya mnara wa Kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa wa Taifa la Zimbabwe katika eneo hilo lililopo kilometa saba kutoka jiji la Harare nchini Zimbabwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mara baada ya kuweka shada la maua katika eneo hilo la makaburi ya mashujaa wa Zimbabwe.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima kabla ya kuweka shada la maua katika eneo hilo la makaburi ya mashujaa wa Zimbabwe.

Mnara wa Kumbukumbu katika eneo la Makaburi ya Mashujaa wa Zimbabwe kama linavyo onekana pichani.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao na Ujumbe wa nchi ya Zimbambwe kilichokuwa kikiongozwa na Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa katika Ikulu ya Harare nchini Zimbabwe tarehe 29/05/2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi kuhusu Kaburi la mmoja wa Mashujaa wa Zimbabwe Herbert Wiltshire Pfumaindi Chitepo ambaye aliuwawa mwezi machi 1975. Marehemu Herbert Wiltshire Pfumaindi Chitepo alikuwa Mkurugenzi wa Mashtaka DPP mweusi wakwanza Tanganyika na Afrika. 

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa  wakizungumza na Wanahabari mara baada ya mazungumzo ya kiserikali katika Ikulu ya Harare nchini Zimbabwe tarehe 29/05/2019

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa  katika picha ya pamoja na Wanahabari  wa Tanzania na Zimbabwe mara baada ya mazungumzo ya kiserikali katika Ikulu ya Harare nchini Zimbabwe tarehe 29/05/2019