Daily Archives: May 17, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za Mwisho katika jeneza lenye Mwili wa Marehemu Dada yake

Picha namba 1-2.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za Mwisho katika jeneza lenye Mwili wa Marehemu Dada yake Gaudensia Felician Marko Msangwa  aliyefariki Dunia leo tarehe 17 Mei 2020, Chato mkoani Geita. Marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho Buzirayombo Chato mkoani Geita.

Picha namba 3. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka msibani katika mtaa wa Msilale Chato mkoani Geita mara baada ya kuaga mwili wa Marehemu Dada yake Gaudensia Felician Marko Msangwa aliyefariki Dunia leo tarehe 17 Mei 2020, Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ASALI IBADA YA JUMAPILI YA TANO BAADA YA PASAKA KATIKA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA(KKKT) USHARIKA WA CHATO MKOANI GEITA LEO TAREHE 17 MEI 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Jumapili ya Tano baada ya Pasaka katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chato mkoani Geita leo tarehe 17 Mei 2020.

.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chato mkoani Geita leo tarehe 17 Mei 2020 mara baada ya Ibada.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi Mchango wake kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa la (KKKT) Usharika wa Chato kiasi cha Shilingi milioni 10 kwa Mchungaji wa Jimbo la Kusini c (Biharamulo) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Kanisa hilo Mch. Thomas Pascal Kangeizi.