Daily Archives: May 29, 2020

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ikulu, Chamwino.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Mei, 2020 amekagua maandalizi ya sherehe za uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma zitakazofanyika kesho tarehe 30 Mei, 2020.

Jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi hizo litawekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Maria Nyerere (kwa niaba ya Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere), Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi na zitarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao.

 

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Picha namba 1-5. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akichota mchanga kuweka kwenye Toroli wakati alipoenda kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo. tarehe 29-05-2020