Daily Archives: July 4, 2020

Taarifa kwa vyombo vya Habari

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Julai, 2020 amemteua Bw. Albinus Mgonya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mgonya alikuwa Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Rukwa na anachukua nafasi ya Bw. Mohamed Musa Utaly.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Waziri Khachi Kombo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kombo alikuwa Afisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro na amechukua nafasi ya Bi. Wendi Ng’ahala
Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 05 Julai, 2020 na wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 06 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi.