Monthly Archives: August 2020

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI AMEKAGUA MAGARI YALIYOTAIFISHWA BAADA YA KUHUSIKA KATIKA MATUKIO YA UHUJUMU UCHUMI.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2020 amekagua magari yaliyotaifishwa baada ya kuhusika katika matukio ya uhujumu uchumi, na kisha kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani Jijini Dodoma.

Idadi ya magari hayo ni 130 yakiwemo makubwa na madogo yalikamatwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kisha wahusika kufikishwa Mahakamani na Mahakama kutoa uamuzi wa kuyataifa.

Akizungumza baada ya kuyakagua, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Jeshi la Polisi na wote waliohusika kuwakamata waliokuwa wanajihusisha na vitendo hivyo (ikiwemo biashara haramu ya meno ya tembo) na ameagiza magari hayo yagawanywe katika taasisi mbalimbali za Serikali ili yatumike kuendesha shughuli za kuwahudumia wananchi na kuzalisha mali.

Mhe. Rais Magufuli pia amewapongeza wananchi waliojitokeza kutoa taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watu waliokuwa wanafanya uhalifu kwa kutumia magari hayo na amewaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kukomesha vitendo hivyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2020 amekagua magari yaliyotaifishwa baada ya kuhusika katika matukio ya uhujumu uchumi, na ameagiza magari hayo yagawanywe katika taasisi mbalimbali za Serikali ili yatumike kuendesha shughuli za kuwahudumia wananchi na kuzalisha mali.Jumla ya magari 130  yamehifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani Jijini Dodoma.

 

 

MHE.RAIS DKT.JOHN.P.MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA DOMINIKA YA 21 YA MWAKA A NA UZINDUZI WA KANISA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulia akipokea michango kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya aliposhiririki iliyotokana na harambee kuchangiau ujenziwa Msikiti wa Chamwino wakati wa Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ambapo pia alizindua Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino Jumapili Agosti 23,. 2020

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulia akiwashukuru kwa  michango ya ujenzi wa Msikiti wa Chamwino wakati wa Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ambapo pia alizindua Kanisa, Nyumba ya Mapadre na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili 23,. 2020Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya, Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania )TEC) Padri Dkt. Charles Kitima na Paroko wa Kanisa hilo Paul Mapalala baada ya kushiriki Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulia akikabidhi michango kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya  Michango hiyo ilitokana na  harambee ya kuchangiau ujenzi wa Msikiti wa Chamwino wakati wa Misa Takatifu ya Dominika ya21 ya Mwaka “A” ambapo pia alizindua Kanisa, Nyumba ya Mapadre  na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata .