Daily Archives: August 5, 2020

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Agosti, 2020 amewasili Dodoma akitokea Jijini Dar es Salaam.

Akiwa njiani, Mhe. Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Dumila katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro ambao wanajishughulisha na biashara ndogondogo za kuuza mahindi ya kuchoma, mahindi mabichi, Nyanya, Vitunguu, mbogamboga na bidhaa nyingine zinazozalishwa katika eneo hilo.

Mhe. Rais Magufuli amekubali ombi la wananchi hao la kupanuliwa kwa barabara na kujengwa kwa vibanda vya biashara katika eneo hilo, kwa kuwa mazingira yaliyopo sasa ni finyu na hatarishi kutokana na kusongamana katika barabara kuu.

Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali itatoa shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vibanda hivyo na pia amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) katika Mkoa wa Morogoro kufanya upanuzi wa barabara katika eneo hilo.

MHE. RAIS DKT. MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA DUMILA DARAJANI MKOANI MOROGORO AKIWA NJIANI KUELEKEA MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia Mhindi wa Kuchoma alionunua kutoka kwa mfanyabiashara mdogo katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.

 

.Wafanyabiashara wa Dumila Darajani wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kusimama katika eneo hilo wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma. Rais amewaahidi kiasi  Cha shilingi milioni mia moja za kujengea vibanda   vizuri vya kufanyia biashara zao katika eneo hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wafanyabiashara  huku ameshikilia Mhindi wa Kuchoma alioununua  wakati akielekea mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono kuwaaga  wafanyabiashara wadogo  katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Mhindi wa Kuchoma kutoka kwa mfanyabiashara mdogo katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.