Daily Archives: November 5, 2020

PICHA MBALI MBALI ZA UAPISHO WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa katika gari maalumu  wakati akiingia uwanja wa Jamhuri stadium kuapishwa urais   kuongoza  kwa awamu ya pili baada  ya kushinda  tena kwa aslimia 84 za kura zote zilizo pigwa katika uchaguzi wa mwaka huu, Mhe rais  Dkt Magufuli ameapishwa  uwanja wa Jamhuri Dodoma  leo tarehe 5 Novemba 2020

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiapa kuongoza nchi kwa awamu ya pili ya miaka mitano,  uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi hati ya kiapo  kwa Katibu mkuu Kiongozi baada ya kumaliza  kuapa  kuongoza nchi katika madaraka ya Rais wa muungano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma

Makamo wa rais mhe. Samia Suluhu  Hassan akiapa mara  baada ya rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kumaliza kuapa mapema leo.

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa majeshi Brigedia jenerali Venance Mabeyo wakati  Mhe rais Magufuli  akikagua  gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake