Monthly Archives: December 2020

Taarifa kwa vyombo vya Habari

UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi (Jaji wa Mahakama ya Rufani) kuwa Kamishna wa Maadili.

Mhe. Mwangesi ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya Jaji wa Mahakama ya Rufani Mstaafu Harold Nsekela kufariki dunia.

Uteuzi wa Mhe. Mwangesi unaanza leo tarehe 23 Desemba, 2020 na ataapishwa kesho tarehe 24 Desemba, 2020 saa 4:00 asubuhi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.