Daily Archives: January 30, 2021

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA MRADI WA MAJI MKOANI TABORA PAMOJA NA UJENZI WA JENGO LA WAGONJWA WA HUDUMA YA DHARURA HOSPITALI YA KITETE MKOANI TABORA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakiondoka mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati akikagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa Maji ya Ziwa Victoria itakayo hudumia miji ya Tabora, Igunga na Nzega.leo tarehe 30 Januari 2021