TANZANIA NA SAUDI ARABIA ZASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA UCHUMI, BIASHARA, UWEKEZAJI, UFUNDI, VIJANA NA MICHEZO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MARCHI 24,2016

24fe4afc-fd9f-4f7e-9566-6cc3c98559e3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 

54418b39-66e3-48b7-88d2-11054190b0d3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja, March 24,2016 Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 

3421f617-7aaf-4396-88c5-eaa3c4fcb8af Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair.

d73e624c-6e46-4e33-97d0-6aaa9d06ad9d Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia kubadilishana hati baada ya uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair

df91a1f9-a99d-4978-892e-efd109efddbf Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Al Jubair, Waziri Mahiga, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kulia) na ujumbe uliombatana na Waziri Al Jubair. 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *