RAIS KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA UZINDUZI WA PROGRAMU YA UIMARISHAJI WA MIPAKA YA KIMATAIFA MKOANI KAGERA AGOSTI 27,2014

1

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

5

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

3

 

4

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakitembelea eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

  6

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipata maelezo na kuangalia vifaa vya upimaji  eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

 7 

 

8sfgc

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

9

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

10

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizindua kwa pamoja eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. 

 

11nnkjggj

 

12

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakichanganya udongo na kujenga kwa pamoja alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.

 13 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na wananchi wa nchi zao wakisimama wakati nyimbo za Taifa za Burundi na Tanzania zikipigwa katika  eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. 

14

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakijipatia chakula cha mchana katika  eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. 

 

15

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiagana katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. 

 

 

MARAIS KIKWETE NA NKURUNZINZA WASHUHUDIA UHAKIKI WA MPAKA WA NCHI ZAO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezitaka Mamlaka zote zinazohusika na Uhakiki Mipaka na Uwekaji Mawe katika Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Burundi na mipaka mingine kati yaTanzania na nchi nyingine unakamilika mapema iwezekanavyo.Aidha, Rais amesema kuwa Tanzania inapima mpaka wake na Burundi na mipaka yake na nchi nyingine jirani siyo kwa sababu ya kuwepo kwa migogoro na nchi jirani bali kwa sababu ya kuwahakikishia wananchi wa nchi zote wanaoishi mipakani kujua ni sehemu gani na mazingira yapi wanafanyia shughuli zao za maendeleo.Rais Kikwete ameungana na Rais wa Burundi, Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza leo, Jumatano, Agosti 27, 2014 kuzindua Zoezi la Upimaji na Uwekaji Mawe ya Mpaka kati ya Tanzania na Burundi katika sherehe kubwa na ya kusisimua iliyofanyika upande wa Tanzania wa Kijiji cha Mpakani cha Mugikomero. Rais Kikwete amewasili Mugikomero saa 8:15 mchana akitokea Uwanja wa Ndege wa Mchauru, mjini Geita ambako ndege yake imetua saa nne kamili asubuhi ikitokea mjini Dodoma kujiunga na Rais Nkurunzinza ambaye alitangulia kuwasili kwenye kijiji hicho. Rais Kikwete amekielezea kitendo cha Uzinduzi wa Zoezi hilo kuwa ni kielelezo tosha cha uhusiano mwema, udugu na urafiki uliopo kati ya Tanzania na Burundi, nchi mbili ambazo pamoja na Rwanda zilikuwa nchi moja zilikuwa chini ya Utawala wa Wajerumani ikijulikana kama German East Africa.Nchi hizo zilitengana baada ya Ujerumani kushindwa katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambako Tanganyika iliwekwa chini ya utawala wa Waingereza wakati Burundi na Rwanda ziliwekwa chini ya himaya ya Ubelgiji. Akifafanua umuhimu wa kuhakiki mpaka, Rais Kikwete amesema kuwa mara ya mwisho kwa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Burundi kuhakikiwa na mkataba kusainiwa kati ya nchi hizo ilikuwa Agosti 5, mwaka 1924, miaka 90 iliyopita.

“Kama zilivyo nchi nnyingine za Afrika, Tanzania na Burundi zilirithi mpaka uliopo kutoka kwa waliokuwa watawala wetu enzi za ukoloni. Mpaka huu haujafanyiwa marekebisho wala kuimarishwa tangu nchi zetu zipate uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita. Katika kipindi hicho yamekuwepo mabadiliko mengi likiwemo ongezeko la watu, shughuli za maendeleo katika maeneo ya mpakani na hata alama za mipaka zimekuwa vigumu kutambulika ama kwa sababu ya kuchakaa au mawe yameng’olewa,” amesema Rais Kikwete.

Ameongeza pia kuwa baada ya kutambua vyanzo vya migogoro na utata miongoni mwa baadhi ya nchi za Afrika, Umoja wa Afrika (AU) katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Serikali kilichofanyika Accra, Ghana Juni 27, mwaka 2007, uliamua kuwa nchi zote zishirikiane kuimarisha mipaka yao ifikapo mwaka 2012. Muda huo uliongezwa hadi 2017. Rais Kikwete amesema kuwa zoezi hilo ambako katika awamu ya kwanza kilomita 120 za mpaka zimepimwa na kuwekewa mawe ya utambuzi wa mpaka, halikuwa rahisi kwa sababu mpaka wa Tanzania na Burundi ni mrefu, kiasi cha kilomita 450, sawa na urefu kati ya Dar Es Salaam na Lindi.

“Isitoshe mpaka hauko mijini, maeneo mengi yako misituni kwenye mabonde na milima. Ni vigumu kuyafikia. Kwa upande wetu, mpaka uko katika mikoa miwili ya Kagera na Kigoma na katika wilaya tano, nne zikiwa katika Mkoa wa Kigoma na moja ikiwa Ngara, Mkoa wa Kagera. Isitoshe, hatuna mfadhili na zoezi hili tumeligharimia sisi wenyewe,” amesema Rais Kikwete.

Rais Kikwete amewambia wananchi kuwa mbali na zoezi na Burundi, nchi ya Tanzania inaendelea na zoezi kama hili kwa nchi nyingine jirani, akisisitiza kuwa mpaka wa Tanzania na nchi za Kenya, Mozambique, Comoro na Shelisheli katika Bahari ya Hindi umefikisha na Mikataba kutiwa saini.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *