RAIS KIKWETE AONGOZA UFUNGAJI WA ZOEZI LA MEDANI LA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA (JWTZ) SEPTEMBER 05,2014 – ARUSHA

unnamed (96)
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia madhara ya mapigo ya silaha mbalimbali wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ Monduli, Arusha, Septemba 5, 2014unnamed (97)

Sehemu ya askari wakitoka katika mapambano wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ Monduli, Arusha, Septemba 5, 2014unnamed (98)

 

 

unnamed (99)

 

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakismama kwa nyimbo ya Taifa  wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ Monduli, Arusha, Septemba 5, 2014unnamed (100)

Askari wa kikosi cha mizinga akichukua taswira meza kuu wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ Monduli, Arusha, Septemba 5, 2014unnamed (92)

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakipata picha ya kumbukumbu na sehemu ya wapiganaji  wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ Monduli, Arusha, Septemba 5, 2014unnamed

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza askari wanawake waklioshiriki katika mapambano wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ Monduli, Arusha, Septemba 5, 2014ro9

Baadhi ya taswira za zoezi la medani la operasheni maliza matata ,zikijumuisha siraha za moto kwa njia ya  ndege za kivita ,vifaru, Makombora na Risasi kwenye sherehe za miaka 50 ya JWTZ  kwenye eneo la angururusu, Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha 

ro11

Baadhi ya taswira za zoezi la medani la operasheni maliza matata ,zikijumuisha siraha za moto kwa njia ya  ndege za kivita ,vifaru, Makombora na Risasi kwenye sherehe za miaka 50 ya JWTZ  kwenye eneo la angururusu, Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha 

ro12

Madhara ya mashambulio hayo  ya mazoezi

 

ro15

Madhara ya mashambulio hayo  ya mazoezij3

Mkuu wa majeshi wa kwanza Jenerali Mirisho Sarakikya akipongezwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati wa kupiga picha za kumbukumbu.  Kulia ni Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akifuatiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi

j7

Picha ya pamoja na Wakuu wa vikosi mbalimbali

j10

Picha ya pamoja na Wakuu wa vikosi mbalimbalij13

Picha ya pamoja na Wakuu wa vikosi mbalimbalij10

 Kumbukumbu na Wakuu wa vikosi vya vifaruj13

 Picha na Viongozi wa vikosi vya Wahandisi medani 
j16

 Kumbukumbu na Makamanda mbalimbali walioishiriki zoezi

 j18

      Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi (wa tatu kushoto) , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kushoto) , Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange (kushoto kwa Rais) , Mnadhimu Mkuu wa JWTZ ,  Luteni  Jenerali  Samwel Ndomba Kamanda wa vikosi vya Ardhini wa  JWTZ  Meja Jenerali Salum Kijuu katuika picha ya kumbukumbu na  Maafisa na askari walioshiriki zoezij26

 Amiri Jeshi Mkuu na Makamanda wakisimama swawa wakati Wimbo wa Taifa unapigwaj27

 Saluti toka kwa makamanda wakuu

 j28

 Makamanda wapiganajij31

Vicheko na bashasha vinatawala wakati Amiri Jeshi Mkuu anapoondoka eneo la Langarurusu huko Monduli, Mkoa wa Arusha,  baada ya kuongoza zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ  lililofana sana.

 j25

 Makamanda walioongoza sherehe hizo kwa weledi wa hali ya juuj23

 

RAIS KIKWETE: HAYA NDIYO MAFANIKIO YA JWTZ

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amelisifia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kutaja mafanikio yake makuu katika miaka 50 ya uhai wake, akisisitiza kuwa ni Jeshi imara na bora linaongozwa na misingi ya uzalendo, utii na nidhamu ya hali ya juu.

Rais pia amesema kuwa kwa amani, utulivu na usalama ambao umekuwepo katika Tanzania kwa miaka 50 iliyopita umechangiwa sana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.  JWTZ lilizaliwa Septemba Mosi, 1964.

Akizungumza na maelfu ya wapiganaji na wananchi kwenye Sherehe za Miaka 50 ya Jeshi hilo kwenye eneo la Langururusu, Wilaya ya Monduli, Mkoa wa Arusha leo, Ijumaa, Septemba 5, 2014, Rais Kikwete amesema kuwa uzalendo na nidhamu  ni mambo ambayo yanalitofautisha JWTZ na majeshi mengine mengi duniani mambo yaliyoyashinda majeshi ya nchi nyingi hususan katika Afrika.

Rais Kikwete alikuwa anazungumza baada ya kushuhudia Zoezi la Medani la Operesheni Maliza Matata ambalo limeshirikisha mamia ya wapiganaji na maofisa  ambako zimetumika silaha za moto kwa njia ya ndege za kivita, vifaru, makombora na risasi.

Zoezi hilo limeshirikisha maofisa na askari kutoka Makao Mkuu ya Jeshi, Kamandi ya Majeshi ya Nchi Kavu, Kamandi ya Jeshi la Anga, Kamandi ya Jeshi la Maji, Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Akiba. Rais Kikwete amewaambia wapiganaji nao na maofisa wao ambao walikuwa ni pamoja na wakuu waliopita wa Jeshi hilo kuwa moja ya mafanikio makubwa ya Jeshi hilo ni kusimamia na kutekeleza majukumu yake iwe ni wakati wa amani ama wakati wa vita, tena kwa weledi mkubwa. Rais Kikwete ameyataja mafanikio machache ya Jeshi hilo kuwa ni pamoja na kushiriki na kufanikisha harakati za Ukombozi Barani Afrika kwa kufundisha majeshi ya Vyama vya Ukombozi, na kushiriki moja kwa moja kwenye vita vya Ukombozi mwa Kusini mwa Bara la Afrika katika Mozambique, Angola, Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini.

Rais pia amesema kuwa JWTZ limelinda uhuru na mipaka ya nchi kwa vitendo kwa kuyapiga majeshi  ya uvamizi ya Idd Amin na kuweka historia kwa kuwa Jeshi lililopigana na jeshi la nchi nyingine na kuliangamiza kabisa.

Mheshimiwa Kikwete pia amesema kuwa JWTZ limeshiriki kikamilifu kwenye operesheni za kulinda amani katika nchi za Liberia, Darfur (Sudan),  Lebanon, Ivory Coast, Visiwa vya Shelisheli, Visiwa vya Comoro na hivi karibuni kuyapiga na kuyatoa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) majeshi ya waasi wa M23. Rais pia amesema kuwa JWTZ limeshiriki kikamilifu shughuli za uokoaji na hususan katika majanga ya ajali kama za Meli za MV Bukoba na kule Zanzibar na kwenye majanga ya mafuriko katika sehemu mbali mbali nchini. Rais amesema kuwa mamilioni ya Watanzania wamenufaishwa na huduma za elimu na afya ambazo Jeshi hilo linazitoa kupitia shule na hospitali zinazomilikiwa na Jeshi na pia limeshiriki katika kukuza elimu ya kujitegemea kwa vijana kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Rais Kikwete amesema kuwa katika miaka yote 50, JWTZ halijawahi kuacha malengo yake makuu ya kuanzishwa kwake. “Limebakia la ulinzi wa wanchi siyo uvamizi. Limebakia Jeshi linalotokana na Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya Wananchi wa Tanzania. Limebakia Jeshi la Ukombozi na kulinda amani lililotumika kwenye harakati za Ukombozi wa Afrika na kulinda amani duniani”.    

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *