ZIARA YA KATIBU MKUU KIONGOZI MKOA WA PWANI KUKAGUA SHUGHULI ZA UTUMISHI WA UMMA KATIKA SEKRETARIETI YA MKOA WA PWANI SEPTEMBER 15,2014

1

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Septemba 15, 2014.

2

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati), akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na baadhi ya watendaji wa Taasisi za Umma zilizopo mkoani Pwani katika kikao alichofanya na watendaji hao. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bibi Mgeni Baruhani na kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Abdallah Sagini, Septemba 15, 2014

3

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Bw. Abdallah Sagini (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zilizotolewa na Watumishi mbalimbali wa Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani na wilaya zake. Kulia ni  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue.

4 (1)

Watendaji kutoka Ofisi ya Rais Ikulu, waliombatana na Katibu Mkuu Kiongozi wakichukua kumbukumbu muhimu katika kikao hicho. Kutoka kushoto ni Bw. Francis Mang’illa, Mratibu wa Utawala Serikalini, Bw. Charles Mwankupili, Katibu Msaidizi wa Baraza la Mawaziri na Bw. Apolinary Tamayamali, Kaimu mratibu wa programu za maboresho serikalini.

4 (2)

Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani na wilaya zake na watumishi wa Taasisi za Umma katika mkoa wa huo wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Elimu Kibaha. Septemba 15, 2014.

6

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Taasisi za Umma Mkoani Pwani. kulia kwa Katibu Mkuu Kiongozi ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Abdallah Sagini na kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bibi Mgeni Baruhani. Septemba 15, 2014.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *