ZIARA YA KATIBU MKUU KIONGOZI MKOA WA TANGA KUKAGUA SHUGHULI ZA UTUMISHI WA UMMA KATIKA SEKRETARIETI YA MKOA WA TANGA SEPTEMBER 16,2014

1-IMG_5220

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya mkoa wa Tanga alipowasili kuanza kuanza ziara ya siku moja mkoani humo kwa ajili ya kukutana na watumishi wa umma, nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Bibi Halima Dendegu. Septemba 16, 2014.

2-IMG_5234

 

 

 

 

 

 

 

 

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, Septemba 16, 2014.

3-IMG_5340

Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, Bw. Salum M. Chima, akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi (hayupo pichani) kuzungumza na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga na wilaya zake pamoja na watendaji wa Taasisi mbalimbali za umma zilizopo mkoani humo, Septemba 16, 2014.

4-IMG_5359

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati), akisisitiza jambo wakati akizungumza na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga na wilaya zake pamoja na watendaji wa Taasisi za umma. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Bw. Abdallah Sagini na Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, Bw. Salum M. Chima Septemba 16, 2014.

5-IMG_5344

Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga na wilaya zake pamoja na watendaji wa Taasisi  za umma zilizopo mkoani humo, wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo.

6-IMG_5379

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (kulia) akisikiliza baadhi ya hoja zilizowasilishwa na baadhi Watumishi wa Umma mkoani Tanga wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa, Septemba 16, 2014.

7-IMG_5407

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Bw. Abdallah Sagini (aliyesimama), akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizowasilishwa kwake na baadhi Watumishi wa Umma mkoani Tanga. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi na kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Bw. Salum M. Chima, septemba 16,2014.

8-IMG_5428

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Sekretarieti ya mkoa wa Tanga mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa, Septemba 16, 2014.

u

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *