ZIARA YA KATIBU MKUU KIONGOZI MKOA WA MANYARA KUKAGUA SHUGHULI ZA UTUMISHI WA UMMA KATIKA SEKRETARIETI YA MKOA WA MANYARA SEPTEMBER 17,2014

IMG_5457

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Manyara Bw. Elaston J. Mbwilo (hayuko pichani), mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Septemba 17, 2014.

IMG_5499

Mkuu wa mkoa wa Manyara Bw. Elaston J. Mbwilo (aliyesimama) akiwasilisha taarifa fupi ya hali ya ulinzi na usalama katika mkoa wa huo kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, aliyekuwa ziarani mkoani humo, septemba 17, 2014.

IMG_5554

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati) akizungumza na Wakurugenzi wa Sekretarieti na Halmashauri za Mkoa wa Manyara pamoja na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma zilizopo mkoani humo. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Bw. Abdallah Sagini na kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara Bw. Omar Chambo, septemba 17, 2014.

IMG_5565

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati) akiwasili katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Manyara kukutana na watumishi wa Seketarieti ya Mkoa na Wilaya zake. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Bw. Abdallah Sagini na kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara Bw. Omar Chambo, septemba 17, 2014.

IMG_5574

Baadhi ya watumishi wa Seketarieti ya mkoa wa Manyara na Wilaya zake ambao walihudhuria kikao kichoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, kuhusiana na masuala mbalimbali ya Utumishi wa Umma, septemba 17, 2014.

IMG_5578

 

Baadhi ya watumishi wa Seketarieti ya mkoa wa Manyara na Wilaya zake ambao walihudhuria kikao kichoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, kuhusiana na masuala mbalimbali ya Utumishi wa Umma, septemba 17, 2014.

IMG_5581

Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara Bw. Omar Chambo, akisoma taarifa fupi ya kiutendaji ya mkoa kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi kuzungumza na watumishi wa Seketarieti ya mkoa wa Manyara na Wilaya zake, septemba 17, 2014

IMG_5587

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati) akizungumza na watumishi wa Seketarieti ya mkoa wa Manyara na Wilaya zake. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Bw. Abdallah Sagini na kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara Bw. Omar Chambo, septemba 17, 2014.

IMG_5590

Mmoja wa Watumishi Seketarieti ya mkoa wa Manyara akiwasilisha hoja yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi na ujumbe wake wakati wa kikao cha Katibu Mkuu Kiongozi na Watumishi hao kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Manyara, septemba 17, 2014.

 IMG_5608

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (wa tatu kutoka kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Sekretarieti ya mkoa wa Manyara mara baada ya kumaliza kikao chake na watumishi hao, septemba 17, 2014.

IMG_5613

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (wa nne kushoto) akisalimiana na baadhi ya watumishi wa hospitali ya mkoa wa Manyara alipotembelea hospitali hiyo kukagua utendaji kazi na maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo.

IMG_5621

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Manyara (kulia) akimwonyesha Katibu Mkuu Kiongozi baadhi ya maeneo ya hospitali ya mkoa huo, katibu Mkuu Kiongozi alitembelea hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo, septemba 17, 2014.

 IMG_5652

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (kushoto) akimjulia hali mtoto Emmanuel Marcel aliyelazwa katika hospitali ya mkoa wa Manyara, kulia ni mama wa mtoto huyo Jovita Petro. Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea hopitali hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Manyara, septemba 17, 2014.

IMG_5657

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

IMG_5667

 

 

 

 

 

 

 

 

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati) akikagua sehemu ya hospitali ya mkoa wa Manyara inayoendelea kujengwa, Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea hopitali hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Manyara, septemba 17, 2014.

IMG_5672

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (wa tatu kulia) akiangalia baadhi ya vifaa vya maabara vya kisasa vya hospitali ya mkoa wa Manyara. Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea hopitali hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Manyara, septemba 17, 2014.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *